Wengi wanadai hawafanyi mazoezi kwa kudai kukosa muda wa mazoezi. Watafiti wamedai mazoezi magumu (high-intensity interval training/HIIT) ya daika 10 tu yanatosha kukuweka mwenye afya njema
UTAFITI: Ulaji samaki unahusishwa na kupata usingizi mnono na pia unahusishwa na kuwa na akili sana kwa watoto wanaokula samaki ikilinganishwa na watoto wasiokula samaki
Wasiwasi ni sehemu ya maisha yetu. Unaweza kupatwa wasiwasi wakati wowote mfano umechelewa mahali, unapouguliwa na mtu unayempenda au unapokuwa na matatizo ya kiuchumi. Watafiti wamedai wasiwasi huweza kuchochea kupanda kwa shinikizo la damu
Vyakula & sharubati (juisi) ya kuondoa sumu vimekuwa na umaarufu mkubwa siku hizi. Wenyewe wanadai vinasafisha damu na kuondoa sumu mwili. Wataalamu wanadai haiko wazi jinsi gani hufanya hivyo & ni sumu gani mahususi zinatolewa
Wengi tunaokutana nao kwa mara ya kwanza huuliza tunafanya kazi gani, tumeoa au kuolewa, tunaishi wapi n.k maswali huwa kama mtu anavyouliza bidhaa za nyumbani dukani ila wengi husau kuuliza swali la msingi, kama tuna furaha au huzuni maishani.
Akili yako hukubali na kuamini chochote unachoiambia. Ilishe akili yako maarifa, ukweli, matumaini na upendo. Akili yako ikiwa na vitu hivi, unaweza kutenda kwa ufanisi bila kuwaaumiza wengine kihisia, kimwili na kiuchumi
Unapodhani huwezi kufanya kitu fulani basi mfumo wa mwili kibaiolojia huanza kudhihirisha kile unachodhani huwezi. Huwezi kufanya kile unachofikiri huwezi kukifanya. Siri ya mafanikio ni pamoja na kujiamini kuwa unaweza na mwisho utaweza.
Furaha huja pale kuna maelewano kati ya kile unachofikiri, unachosema na kufanya. Kuendelea kufikiri tu bila kufanya unachofikiri hakuleti matokeo unayoyatamani na pia kufanya bila kufikiri kunaweza leta matokeo hasi.
Ili tuwe na afya nzuri ya kimwili, ni lazima tule na chakula chenye lishe na kufanya mazoezi kwa ukawaida. Vivyo hivyo, ili tuwe na afya nzuri ya kiroho ni lazima tujilishe chakula cha kiroho chenye lishe na kuonyesha kwa ukawaida kwamba tuna imani kwa Mungu.
Yeyote anayeacha kujifunza ni mzee bila kujali ana miaka 20 au 80. Mtu anayejifunza kila siku hubaki kijana. Kitu kikubwa maishani ni kuendelea kkuweka ubongo wako kwenye ujana
Pesa inaweza isikununulie furaha ila inaweza ikakununulia muda zaidi wa kuitafuta furaha. Watafiti wamegundua watu wenye vipato vikubwa wanaweza kuishi umri mrefu zaidi kuliko wenye vipato vidogo
Kati ya tukio na muitikio wako juu ya tukio lilitokea kuna nafasi. Nafasi ya kuamua nini cha kufanya. Uamuzi mzuri unakupa nguvu na uhuru ila uamuzi mbaya unaweza kuharibu amani ya moyo & akili kwako au kwa wengine
Kuwa na mkazo (stress), hisia kali kama furaha (kucheka sana), tabia kama kula sana, kula haraka sana, kunywa vinywaji vinavyofanya tumbo kujaa gesi kama soda huchangia mtu kupata kwikwi
Baada ya kufanya mazoezi unahisi mwili umechangamka kwa sababu mapigo ya moyo huongezeka kitu kinachomaanisha ongezeko la mzunguko wa damu & oksijeni kwenye ubongo
Kiharusi (Stroke) husababisha viungo vya mwili kupooza kutokana & kuvuja damu au kuziba kwa mshipa wa damu katika ubongo. Kiharusi humkumba mtu yeyote lakini watu wazima wenye umri kuanzia miaka 40 na kuendelea ndiyo hushambuliwa zaid