Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Pili, alitaka kuhimarisha uhusiano na vyama vya wafanyakazi ambao walikuwa wanatishia kugoma kwa mara ya kwanza
. •Tatu, ilikuwa kurekebisha mahusiano mabaya na wahisani kuhusiana na kushamiri kwa rushwa.
•Nne, alitaka kurudisha uhusiano na mashirika ya fedha ya kimataifa ambao walikuwa wamekataa kuanzisha miradi mipya.
•Mwisho aliwapima hao waliokuwa wamechukua fomu akaona atajilaumu hapo baadae kama naye hata gombea.
 
Mwalimu alimshukuru, akamwambia hakuwazakuwa nae angegombea, alikuwa anamfikiria mtu mwingine ambaye alikuwa anasita sita. Akamwambia hatamzuia kama amefanya uamuzi huo. Mwalimu aliwaomba watu kadhaa kumuunga mkono, Mwalimu alipenda hasa uwezo wake wa kufanya maamuzi, Mwalimu alishiriki katika kampeni ambapo Mheshimiwa Mkapa alisisitiza ilani, sio mambo binafsi.
 
11November 23, 1995 aliapishwa kuwa Rais. Katika kuunda Baraza la Mawaziri, Mwalimu alikataa kujihusisha hakuwa muingiliaji –interventionist. Mheshimiwa hakuwa mgombea wa mtu kwa hivyo hakuna aliyetegemea fadhila. Hali ya nchi ya uchumi ilikuwa mbaya sana lakini anasema sikuogopa, kiongozi lazima awe jasiri. Alikumbana na uzembe, kutowajibika na rushwa
 
Kazi kubwa -kwanza ilikuwa kuwashawishiwahisani kuwa mambo yatabadilika. Nchi ilikuwa na madeni makubwa sana. Deni letu lilikuwa dola bilioni saba, tulisamehewa bilioni tatu, hii ilikuwa hatua kubwasana na ilimfurahisha Mwalimu ambaye alishaanza kuumwa.Mheshimiwa aliamini tulihitaji kujiangalia upya na kujifikiria kimkakati upya namna tulivyo kuwa tunaendesha nchi
 
Matokeo yake ni kwamba mapato yaliongezeka karibu mara tatu kutoka dola 612,587 mwaka 1995 kufikia dola 1,796,862 miaka kumi baadae. Fedha za kigeni ziliongezeka kutoka uwezo wa kununua bidhaa za mwezimmoja na nusu kufikia uwezo wa kununua bidhaa za miezi mitano na theluthi moja. Riba za benki ilishuka kutoka asilimia 36% kufikia asilimia 15% mwaka 2005
 
Ilianzishwa TRA kuimarisha ukusanyaji wa mapato Julai 1996
. •Ukaanzishwa mfumo wa VAT Julai 1998
•Public Service and Act pamoja na Public Procurement Regulatory Authority vilianzishwa 2001
•Commision for Human Rights and Good Governance ilianzishwa Julai 2001
•Prevention of Corruption Bureau nayo ilianzishwa, Mheshimiwa akaitwa Mr clean
 
Regulatory Agencies nyingine zilianzishwa nyingi ikiwa ni pamoja na Brela, EWURA, TCCRA,SUMATRA, Viwanja vya ndege,Maji safi na taka, TANROADS,na National Business Council kuhimarisha mahusiano na wafanya biashara.

Kati ya mageuzi tuliyofanya yaliyokuwa na utata sana ni kubinafsisha mashirika ya Umma, mageuzi/maboresho ya utumishi, na uuzaji wa nyumba za Serikal
 
Mheshimiwa Mkapa anabainisha kuwa, lakini Mwalimu hakunisema ana sijui kwa nini, ukweli ni kwamba Mwalimu alikuwa pragmatist na aliona hali halisi. Kwa bahati mbaya sikufuatilia utendaji wa mashirika Mheshimiwa Mkapa anaendelea mashirika tuliyo yaabinafsisha kama ambaavyo nilivyofanya kwa Regulatory Agencies. Pia kweli kuwa tulibinafsisha kwa watu wan je kuliko wazawa
 
Pamoja na ugumu na utata wa baadhi ya mageuzi kura zakekatika uchaguzi wa mwaka 2000 ziliongezeka kwa asilimia 100%. Hii kwakeilikuwakuambiwa “Songa mbele, endelea”Na niliendelea, anasema.

Mheshimiwa Mkapa anasimulia kuwa maono yake: ni maisha ya hali ya juu, amani, utulivu na umoja, utawala bora,jamii iliyoelimika na uchumi shindani wenye uwezo wa kukua kiendelevu na mgawanyo shirikishi wa kipato.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…