Watu hawa ,wengine ambao bado wapo hai ilhali wengine wamefariki wakati mmoja walionekana kuwa kileleni mwa taaluma zao za uhalifu .Ujanja wao na weledi wao kutafuta pesa na kukwepa mkono wa sheria ulionekana kama ushujaa na hadi leo katika baadhi ya nchi wangali wanachukuliwa kama 'mashujaa' .
Hatahivyo walikumbana na mauti yao katika hali ambazo pesa na mali walizokuwa wametengeza hazingeweza kuwasaidia .Hawa hapa baadhi ya wahalifu sugu waliokuwa na utajiri ambao walipata kupitia uhalifu na ulaghai
Baada ya Marekani kutoa amri ya kukamatwa kwake ili ashtakiwe nchini humo , Escobar alipinga kukamatwa na genge lake lililenga wanasiasa, polisi na waandishi wa habari
Baada ya kukamatwa mnamo 1991, Escobar aliwekwa ndani ya gereza la muundo wake mwenyewe, kwa jina Kanisa Kuu, ambapo aliendelea kusimamia kundi la Medellín
Kwa jumla, Escobar anafikiriwa kusababisha vifo vya takriban watu 4,000.Lakini hali yake ya kuwapenda na kuwasaidia watu wake ilimfanya kuwa maarufu kati ya Wakolombia wengine ambao msaada wao aliuendeleza kwa kutoa pesa nyingi na kuwekeza katika vitongoji duni huko Medellín
Inasemekana kuwa wakati kilele cha nguvu zake katika biashara hiyo haramu Escobar alikuwa mtu wa saba kwa utajiri duniani huku kundi lake la Medellin likidhibiti asilimia 80 ya soko la kokeni ulimwenguni.zaidi ya miaka thelathini baada ya kifo chake ,Escobar yungali anatengeza pesa na huenda sehemu y mali yake bado ipo hadi leo
Septemba mwaka wa 2020 mpwa wa Escobar alisema alipata mfuko wa plastiki na pesa zenye thamani ya $ 18m (£ 14m) zilizofichwa kwenye ukuta wa nyumba moja ya mjomba wake.
Alisema haikuwa mara ya kwanza kupata pesa mahali ambapo mjomba wake alikuwa akijificha ili kuepuka kukamatwa, kwani Escobar aliripotiwa kuficha mali ya thamani ya mamilioni ya pesa
Alikufa katika ufyatulianaji wa risasi na polisi mwaka wa 1993.Nicolás Escobar alikiambia kituo cha Televisheni cha Red + Noticias cha Colombia pia alikuwa amepata mashine ya chapa , simu za setilaiti, kalamu ya dhahabu, kamera na filamu ambayo bado haijatengenezwa.
Baadhi ya noti za miongo kadhaa zilikuwa zimeoza na hazitumiki tena, alisema Nicolás Escobar, ambaye amekuwa akiishi katika nyumba hiyo kwa miaka mitano.
Bernie Madoff, ni bwenyenye wa Wall Street aliyeaibishwa baada ya kukiri kutelekeza moja ya utapeli mkubwa katika historia ya kifedha ya Marekani na amekufa gerezani akiwa na umri wa miaka 82 wiki moja iliyopita.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.