Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Watu hawa ,wengine ambao bado wapo hai ilhali wengine wamefariki wakati mmoja walionekana kuwa kileleni mwa taaluma zao za uhalifu .Ujanja wao na weledi wao kutafuta pesa na kukwepa mkono wa sheria ulionekana kama ushujaa na hadi leo katika baadhi ya nchi wangali wanachukuliwa kama 'mashujaa' .
 
Kwa jumla, Escobar anafikiriwa kusababisha vifo vya takriban watu 4,000.Lakini hali yake ya kuwapenda na kuwasaidia watu wake ilimfanya kuwa maarufu kati ya Wakolombia wengine ambao msaada wao aliuendeleza kwa kutoa pesa nyingi na kuwekeza katika vitongoji duni huko Medellín
 
Inasemekana kuwa wakati kilele cha nguvu zake katika biashara hiyo haramu Escobar alikuwa mtu wa saba kwa utajiri duniani huku kundi lake la Medellin likidhibiti asilimia 80 ya soko la kokeni ulimwenguni.zaidi ya miaka thelathini baada ya kifo chake ,Escobar yungali anatengeza pesa na huenda sehemu y mali yake bado ipo hadi leo
 
Alikufa katika ufyatulianaji wa risasi na polisi mwaka wa 1993.Nicolás Escobar alikiambia kituo cha Televisheni cha Red + Noticias cha Colombia pia alikuwa amepata mashine ya chapa , simu za setilaiti, kalamu ya dhahabu, kamera na filamu ambayo bado haijatengenezwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…