Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Ingawa uhalifu ambao Bernie alihukumiwa kufanya umefafanua ni mtu wa aina gani - pia alikuwa baba na mume. Alikuwa mzungumzaji laini na msomi. Bernie hakuwa mkamilifu. Lakini hakuna mtu aliye sawa." Taraifa hiyo iliongeza.

Bwana Madoff, mtoto wa wahamiaji wa Uropa ambaye alikulia New York, alianzisha kampuni yake ya jina Bernard L Madoff Investment Securities mnamo 1960.
 
Kampuni hiyo ikawa moja wapo ya wafanyabiashara wakubwa - wanunuzi wakiunganishwa na wauzaji wa hisa - na Bwana Madoff aliwahi kuwa mwenyekiti wa soko la hisa la Nasdaq.

Kampuni hiyo ilichunguzwa mara nane na Tume ya Usalama na Ubadilishaji ya Marekani kwa sababu ilipata faida kubwa kupindukia

Walimu wa shule, wakulima, fundi mitambo na wengine wengi pia walipoteza pesa.

"Tulifikiri alikuwa Mungu. Tuliamini kila kitu mikononi mwake," mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel Elie Wiesel, ambaye wakfu wake ulipoteza dola milioni 15.2, alisema mnamo 2009
 
El Chapo Guzman
El chapo Guzman ambaye kwa sasa anahudumia kifungo cha jela nchini Marekani alijiundia sifa kwa kutoroka gerezani Zaidi ya mara moja katika hali za kutatanisha .Hata hivo kikubwa kumhusu ni jinsi alivyotengeza kiasi kikubwa cha apesa kupitia biashara haramu za ulanguzi wa dawa za kulevya

Alianza kujihusisha na uhalifu uliopangwa akiwa na umri wa miaka 15, wakati alipanda bangi katika shamba lake pamoja na binamu zake. Kisha, akachukua jina la utani "El Chapo" - jina la Mexico kumaanisha 'mtu mfupi', Lakini matamanio yake yalidhihirisha kimo chake cha kupungua (yeye ni ana kimo cha futi 5 na nchi 6 , au mita 1.64).
 
Akiwa na umri wa miaka 20, Guzmán aliondoka La Tuna kutafuta utajiri wake katika magendo ya dawa za kulevya. "Daima alipigania maisha bora," mama yake alisema.

Wazazi wake - Emilio Guzmán Bustillos na María Consuelo Loera Pérez - walipata riziki yao kwa kilimo. Baba yake alikuwa mfugaji rasmi lakini inaaminika alikuwa mkulima wa Opium , Malcolm Beith anaandika katika kitabu chake, The Last Narco.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…