Msongo wa mawazo unasababisha kuvurugika kwa homoni za kike: Ovary ni mfuko wa mayai ya kike, yaani mahali ambapo mayai ya kike huzalishwa.Polycstic ovary syndrome au PCOS kwa kifupi ni ugonjwa unaosababishwa na kuvurugika kwa vichocheo vya kike unaowapata zaidi wanawake walioko katika kipindi cha kuzaa. Wanawake wenye PCOS huwa na ovary zilizotanuka na zenye vimbe za majimaji ndani yake. Hedhi isiyokatika au isiyo na mpangilio maalumu, uotaji wa vinyweleo vingi kupita kiasi, kitambi na nyama uzembe, hizi ni dalili ambazo zinaweza kutokea kwa mwanamke mwenye PCOS. Msongo wa mawazo husababisha mwili kutoa vichocheo kama androstenedione ambacho ni kisababishi cha awali cha tatizo cha kujaa majimaji mifuko ya mayai kwa wanawake.