Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mechi ya marudiano lini kamanda? Nawaombea mchomoe kwa niaba ya taifa. Lakini mpunguze kujiamini, maneno na dharau hasa yule msemaji wenu dah! [emoji51][emoji51][emoji51]
boss wao sasa eti alipanga kujinunulia gari za bei mbaya baada ya kipigo kahairiaha kujipa zawadi yupo busy kuwahaidi wachezaji kila goli milion kadhaa
 
Athari za Msongo wa MawazoMsongo wa mawazo unasababisha uzito mkubwa na kitambi: Kuongezeka ovyo kwa uzito,kitambi na nyama uzembe ni tatizo linalohusiana na ,msongo wa mawazo. Msongo wa mawazo unabadili jinsi mafuta yanavohifadhiwa ndani ya mwili kwa sababu ya kubadilika kwa vichocheo na kemikali mbalimbali zinavyozalishwa na mwili pale ambapo unakuwa na stress. Kwa mfano tafiti zinasema kuwa stress kupitiliza husababisha uzalishaji wa protini inayoitwa betatrophin ambayo ni kizuizi kwa vimeng’enya mafuta yaliyohifadhiwa kwenye mwili.
 
Msongo wa mawazo unasababisha kuvurugika kwa homoni za kike: Ovary ni mfuko wa mayai ya kike, yaani mahali ambapo mayai ya kike huzalishwa.Polycstic ovary syndrome au PCOS kwa kifupi ni ugonjwa unaosababishwa na kuvurugika kwa vichocheo vya kike unaowapata zaidi wanawake walioko katika kipindi cha kuzaa. Wanawake wenye PCOS huwa na ovary zilizotanuka na zenye vimbe za majimaji ndani yake. Hedhi isiyokatika au isiyo na mpangilio maalumu, uotaji wa vinyweleo vingi kupita kiasi, kitambi na nyama uzembe, hizi ni dalili ambazo zinaweza kutokea kwa mwanamke mwenye PCOS. Msongo wa mawazo husababisha mwili kutoa vichocheo kama androstenedione ambacho ni kisababishi cha awali cha tatizo cha kujaa majimaji mifuko ya mayai kwa wanawake.
 
Chunguza ratiba yako:

Itazame kwa kina ratiba yako, majukumu yako na kazi ulizojipangia kwa siku. Kama mambo ni mengi mno, yagawanye kwenye makundi ya yale ambayo ni lazima yafanywe na yale ambayo ni muhimu kufanyika. Yale ambayo si ya lazima sana yaweke chini kabisa kwenye ratiba au yaondoe kabisa.
 
Badili Mazingira ya chanzo:


Kama inashindikana kukwepa chanzo cha msongo wa mawazo, badilisha mazingira yake. Jaribu kufikiria ni nini cha kufanya ili chanzo hicho kisijitokeze tena hapo baadaye, hii inamaanisha kubadili namna yako ya mawasiliano au namna unavyoendesha shughuli zako.
 
Tumia muda wako vizuri:

Kushindwa kutumia muda wako vizuri ni chanzo kikubwa cha kupata msongo wa mawazo. Unapokuwa umechelewa kukamilisha jambo lako, utalifanya bila utulivu na utakosa umakini. Lakini ukiwa na mpango mzuri wa muda wako, utafanya kila kitu mbele yako kiufanisi na bila kupatwa na msongo wa mawazo.
 
Mechi ya marudiano lini kamanda? Nawaombea mchomoe kwa niaba ya taifa. Lakini mpunguze kujiamini, maneno na dharau hasa yule msemaji wenu dah! [emoji51][emoji51][emoji51]
Mechi itakuwa jumamosi.

Yale maneno ya shombo na kujiamini ndiyo chereko chereko za mchezo wa soka.
Mchezo wa soka lazima uende kwa kukamiana, kuchimbiana mikwara nk.
 
Kitazame chanzo kwa mazuri yake:

Kitazame chanzo cha kero kwako kwa kutazama mazuri ambayo yanaweza kupatikana kutokana na chanzo hicho. Badala ya kulalamika na kukasirika kutokana na foleni ya magari, chukulia kuwa huo ndio muda mwafaka kwako kujipumzika au kusikiliza muziki unaaoupenda ndani ya gari yako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…