Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kwa kipindi kirefu cha mwaka uliopita 2020, wachezaji walio katika nafasi nzuri walitengwa, wakifanya kazi kwa mshahara wa kiwango cha chini, wakishiriki katika michezo tofauti mbele ya viwanja visivyo na mashabiki hali iliolenga kukabiliana na mlipuko wa virusi vya corona ambao umewanyima mabilioni ya dola wanariadha hao.
 
Wachezaji 10 wanaolipwa fedha nyingi zaidi duniani walipokea kitita cha $1.05 b kupitia mishahara yao katika kipindi cha miezi 12 iliopita, ikiwa ni zaidi ya asilimia 28 ya wale waliopokea fedha nyingi Zaidi 2018, ikiwa ni dirisha la miezi 12 ambalo bondia Floyd Mayweather alijipatia $285 million, zote akizipata katika pigano la maonesho la 2017 dhidi ya Conor McGregor.
 
.Conor McGregor {$180m}Mwaka huu , McGregor amewashangaza wengi kwa kufanikiwa kukusanya dola milioni 180 katika kipindi cha miezi 12 iliopita baada ya kutumia umaarufu wake katika mchezo wa UFC kufungua biashara mbali na kufanya mauzo. Kiasi kikubwa cha fedha hizo kinatoka katika mauzo ya hisa zake katika pombe ya Whiskey ambapo alijizolea $150 million. Ni mara ya kwanza kwa mwanamieleka huyo kuchukua nafasi ya kwanza na mara yake ya pili katika orodha ya wanariadha kumi bora duniani mwaka 2018 ambapo alikuwa katika nafasi ya kujipatia $99 katika pigano lake na Mayweather.McGregor anataka kuwekeza pato lake zaidi akatika pombe . Amewasilisha wazo la kutaka kuinunua klabu ya Manchester United , timu yenye thamni ya juu zaidi katika ligi ya Premia
 
Mchezaji wa pili bora duniani baada ya McGregor ni mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi. Lionel Messi aliuweka ulimwengu wa soka katika ati ati mwaka uliopita alipojaribu kuondoka katika klabu ya Barcelona, suala lililoongezwa nguvu na kandarasi iliofichuliwa iliomuonesha akilipwa fedha nyingi na klabu hiyo zaidi ya vile watu walivyotarajia.
 
Cristiano Ronaldo alikuwa mtu wa kwanza duniani kupata wafuasi milioni 500 duniani katika mtandao wa facebook, Instagram na Twitter mwezi Februari na kufuatilizia hilo mwezi mmoja baadaye kwa kumpita nyota wa zamani wa Brazil Pele kwa ufungaji wa mabao alipofikisha magoli 770 katika mashindano yote mbali na kufunga hat-trick katika mechi dhidi ya Cagliari .
 
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 36 ambaye kandarasi yake ya miaka minne ina thamani ya $64m kila mwaka na inakamilika 2022 , ana kandarasi ya ufadhili na kamapuni ya Nike na ndiye mmiliki wa biashara ya nguo ya CR7, hoteli na maeneo ya kufanyia mazoezi.
 
Bonasi ya $66 milioni aliyowasili nayo pamoja na kandarasi ya miaka minne ilio na thamani ya $160m inamsukuma nyota wa Dallas Cowboys Dak Prescott katika klabu ya watu wenye thamani ya $ 100 milioni wakati anaporudi kutoka katika jeraha la kifundo cha mguu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…