Binadamu tunatofautiana katika uwezo wetu wa kuyapokea, kuyakabili, kuyavumilia, kuyakadiria na kuyasimulia maumivu yetu. Epuka kulinganisha maumivu yako na ya wengine, ama kuyakadiria maumivu ya wengine. Heshimu maumivu ya watu. Maumivu hayana sare. Maumivu hayalinganishiki.