Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Binadamu tunatofautiana katika uwezo wetu wa kuyapokea, kuyakabili, kuyavumilia, kuyakadiria na kuyasimulia maumivu yetu. Epuka kulinganisha maumivu yako na ya wengine, ama kuyakadiria maumivu ya wengine. Heshimu maumivu ya watu. Maumivu hayana sare. Maumivu hayalinganishiki
 
Ujasiri uko wa namna mbili, ujasiri wa leo yako bila ya kujali kesho yako, na ujasiri wa kesho yako bila ya kufurahisha leo yako. Ni maamuzi tu ya kutafsiri nyakati kwa kipimo cha nyakati. Ukijua kupima nyakati kwa kipimo cha nyakati hutopata shida kwa nyakati zozote. PIMA
 
Makovu yetu hubeba taarifa muhimu za historia, huzuni, mafunzo, majuto, hasira na hata usongo wetu. Kadri tunavyoanika makovu yetu tukitafuta kujitetea, huruma na uhalali, tunawapa wabaya wetu silaha dhidi yetu. Sisi si kitu zaidi ya simulizi ya makovu yetu. Tusitiri makovu yetu.
 
Fanya uwezavyo katika maisha yako na hasa katika duru la watu wako wa karibu uwe na walau mtu mmoja anayeweza kukuuliza maswali magumu, machungu na usiyoyapenda.Huyu ndio mhimili wako wa kukuepusha na kufanya makosa, maamuzi mabaya na majuto huogopa sana mtu asiyewajibika kwa mtu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…