Waliofaidika na wewe ukiwa kileleni hugeuka kuwa watesi wako ama wa kwanza kukukimbia unapoanguka. Shukuru Mungu kwa kukuonesha ukweli/uhalisia wa walimwengu kisha songa mbele. Mungu atakuletea watu usiotarajia wa kukuokoa, kukuinua na kurejesha matumaini yako
Maisha ya binadamu ni kama nguo kama hukukatwa basi ulishonwa ukiepuka hilojapo utafungiwa fundo kukunjwa ama kupigwa pasi.Tuko wa aina ukubwa na rangi tofauti kwa mahitaji tofauti.Kila umuonaye na majeraha maumivu yake nyuma ya muonekano wake.Hakuna aliyenusurika
Pengine ni kweli kuwa hakuna linalowezekana katika mazingira yote, lakini katika kila mazingira kuna linalowezekana. Usitafute kisingizio cha kutofanya lolote. Fanya lile linalowezekana katika mazingira yaliyopo. Hakuna mazingira ambayo hakuna lolote linalowezekana.
Njia ya uponyaji inaweza kuambatana na maumivu pia. Kwani hata nguo hushonwa kwa kutobolewa na sindano. Ukiona nguo imependeza, imeshonwa. Ukiona mtu imara na mwenye furaha, kafumwa kwa maumivu mengi.