Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

FB_IMG_1612974617907.jpg
 
Ni biashara
Hakuna mtu atakayetoka China, India au Marekani ili aje Afrika kukugawia mamilioni ya bure kwa njia ya michezo ya kubahatisha ili utoke kwenye umasikini.

Kampuni za michezo ya kubahatisha zinazalisha faida kubwa tena kubwa sana ambayo hufichwa nyuma ya vijizawadi wanavyotoa kwa washindi wa michezo hiyo.
 
Kwa mfano watu 100,000 wakicheza mchezo mmoja kwa shilingi 20,000 pekee ni sawa na shilingi 2,000,000,000; hebu jiulize kweli katika bilioni 2 watashindwaje kutoa zawadi ya milioni 50 hata mara 5?

Naamini umeona wanavyopata faida kubwa kwenye biashara hii ambayo huwadanganya watu kuwa ni njia ya kuwatoa kwenye umaskini.
 
Kumbuka kuwa hivi leo biashara mbalimbali za hovyo hujificha kwenye kofia ya kutambulika kisheria na kulipa kodi. Zipo nchi ambazo zimerasimisha biashara za madawa ya kulevya na silaha kwa kigezo cha kutambulika kisheria na kulipa kodi. Hivyo kuwa macho na michezo ya kampuni hizi kwani ni biashara ya kuwahadaa watu watoe pesa zao.
 
Hakuna mifumo inayoeleweka
Michezo hii haina mifumo wazi na inayoeleweka, wanakuambia cheza mara nyingi ushinde lakini hawasemi ni mara ngapi na ni kwanini wanashinda hata waliocheza mara chache.

Michezo hii huendeshwa kwa mfumo wa kompyuta wa kimahesabu ujulikanao kama probability; hivyo mtu yoyote anaweza kushinda au kushindwa.
 
Hukuathiri na kukuteka kisaikolojia
Michezo ya kubahatisha imetengenezwa kwa njia ambayo inawahadaa na kuwateka wale wanaocheza michezo hiyo. Hivyo huwafanya washindwe kuacha au kujitoa maraa baada ya kuanza kucheza hata kama hawashindi.
 
Kwa mfano michezo hii hukufanya ushinde kiasi kidogo cha fedha baada ya muda fulani ili uamini kuwa utashinda kiasi kikubwa kama utaendelea kucheza. Lakini hii ni mbinu tu ya kukuteka kwani utajikuta umeshacheza sh. 50,000 lakini umeshashinda sh. 5,000 pekee; huoni hapo unaibiwa?
 
Ni vyema ukawekeza pesa zako au hata ukanunua kitu cha maana ambacho kitakufaa kwenye maisha yako. Unaweza kuwekeza pesa zako kwenye mradi au ukanunua vitu kama vile vyombo na vifaa vya majumbani, vitabu au hata kuwasaidia wahitaji kwa muda na pesa zako.
 
Sio suluhisho la uhakika la kifedha
Watu wengi hufikiri kuwa pesa nyingi au zinazopatikana ghafla ndio utatuzi wa matatizo yao. Hebu nikuulize swali, je ulishawahi kuona watu waliokuwa mamilionea lakini leo wanaomba hata ugali wa mchana? Walikuwa na maduka, magari, majumba lakini leo hawana kitu, je hivi vimekwenda wapi?

Pesa ni lazima zikutane na fikra na mikakati sahihi, ukipewa pesa nyingi leo kama huna fikra sahihi hazitakusaidia kitu.
 
Back
Top Bottom