Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"


20210607_201915.jpg
 
Kuna visa vingi vinavyodai kuwa alikuwa vizuri sana kwenye ile tekinolojia ya Kiafrika. Eti alikuwa akiingia ofisini anarusha tu koti au kofia yake na inadata hewani. Kwamba eti alikuwa anaogopwa sana huko Kigoma...
Inadaiwa mbunge kipenzi cha wana Kigoma mjini, marehemu Rajab Omar Mbano, aliyehudumu kati ya 1990-1992, kwamba yeye huyo jamaa ndiye aliyemzimisha kwa sababu za kisiasa.
Hata hivyo mashuhuda wanasema ulozi wake uligonga kisiki kwa mwana Kigoma mwingine Arcado Ntagazwa.
Inadaiwa Ntagazwa alishindikana kwakuwa wilaya ya Kibondo alikotokea Ntagazwa ndiko kwenye Tanuri kuu la kupika UCHAWI.
Hii kwa mujibu wa WAHA wenyewe [emoji2089][emoji2089][emoji2089][emoji2089]
 
Chrisant Majiyatanga Mzindakaya
Kati ya mwaka 1996-1997, akiwa mbunge wa Kwela mkoani Rukwa, Alitikisa vilivyo serikali ya Mkapa.

Kutokana na uhodari wake wa kisiasa alifanikiwa kuukamata mtandao wa rushwa uliokuwa unaratibiwa na wamiliki wa Viwanda vya minofu ya samaki Mwanza na wenye Viwanda vya mafuta ya kula jijini Dar es salaam.
Rushwa ya sh milioni 900 imelipwa kwa aliyekuwa Waziri wa Fedha Profesa Mbilinyi, Aliyekuwa Waziri wa Viwanda dr Juma Ngasongwa na Naibu waziri Fedha wa wakati huo Kilontsi Mpologomyi.
Dr Mzindakaya ambaye wakati huo alidhalaulika kutokana na elimu yake, aliichachafya vilivyo serikali ya Mkapa.
Hali hiyo ilipelekea kuondolewa madarakani Mawaziri wawili na manaibu watatu.

Pumzika kwa amani mwamba Mzindakaya
FB_IMG_1623088350256.jpg
 
Back
Top Bottom