Meneja wa Real Madrid Carlo Ancelotti amewaarifu mabosi wa klabu hiyo kumsajili mshambuliaji wa Chelsea, mjerumani Timo Werner (25). (Fichajes, via Express)
Kiungo wa kihispania, Juan Mata, 33, atalazimika kuchukua mshahara kiduchu wa £70,000 kwa wiki kama anataka kuendelea kusalia Manchester United baada ya mkataba wake kumalizika mwishoni mwa mwezi huu. (Star)
Meneja wa Arsenal, Mikel Arteta yuko tayari kumuuza mlinda mlango, raia wa Ujerumani Bernd Leno (29), msimu huu kama atapatikana mbadala wake. (Mirror)
Chelsea imeongeza dau kwa ajili ya kumnasa mlinzi wa Inter Milan, raia wa Morocco Achraf Hakimi, ikiwemo kitita taslimu cha £43m pamoja na kumtoa nyota wa kimataifa wa Italia Emerson Palmieri (26). (Corriere dello Sport, via Express)
Mwenyekiti wa Klabu ya Tottenham Daniel Levy amesema atafanya 'kile kilicho sahihi kwa klabu' kuhusu masuala ya usajili, ikiwemo mustakabali wa mshambuliaji Harry Kane, aliyeonyesha nia ya kutimka msimu huu. (Goal)
Liverpool inaongoza mbio za kuwania saini ya beki wa Juventus, Cristian Romero raia wa Argentina, ambaye awali alihusishwa na mipango ya kumtimkia Manchester United, baada ya kuonyesha kiwango kizuri akichezea Atalanta kwa mkopo. (Calciomercato - via Team Talk)
Mlinda mlango wa Hispania David de Gea, 30, inaelezwa kwamba hajui hatma yake ndani ya Manchester United wakati huu akijiandaa kufanya mazungumzo na kocha wa mashetani hao wekundu Ole Gunnar Solskjaer kuhusu mustakabali wake ndani ya Old Trafford. (Mirror
Southampton na West Ham ni vilabu vya hivi karibuni kutoka ligi kuu ya England kuhusishwa na mipango ya kumsajili mshambuliaji wa Boavista Alberth Elis (25), huku vilabu vya Brighton na Watford awali vilionyesha pia nia yao ya kumnasa nyota huyo wa kimataifa wa Honduras. (A Bola - in Portuguese)
Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania alifanya mabadiliko ya kiutendaji ikiwa ni pamoja na kumuondoa aliyekuwa Katibu Mkuu kiongozi Dokta Bashiru Ali na kumteua kuwa mbunge. Je, wachambuzi wanazungumzia vipi hatua hii? Msikilize mchambuzi wa siasa za Tanzania, Pascal Mayalla akichambua kwa kina...
Amefanya Mambo mengi mazuri hasa katika kuleta Mandeleo ya Soka Tanzania Katika Wagombea wote waliochukua Fomu Karia ni bora na anafaa kuliko wengine. Tena ikiwezekana na Katiba ikiruhusu Wallace Karia aongoze Milele tu TFF kwani kafanya makubwa. Ukiona Mtu anakubaliwa na GENTAMYCINE jua ni...
Southampton na West Ham ni vilabu vya hivi karibuni kutoka ligi kuu ya England kuhusishwa na mipango ya kumsajili mshambuliaji wa Boavista Alberth Elis (25), huku vilabu vya Brighton na Watford awali vilionyesha pia nia yao ya kumnasa nyota huyo wa kimataifa wa Honduras. (A Bola - in Portuguese)
Klabu ya Borussia Dortmund itatumia kipengele maalumu kuhuisha mkataba wa Jude Bellingham atakapotimiza miaka 18 baadae mwezi huu, ili kiungo huyo wa England asalie katika klabu hiyo ya Bundesliga mpaka mwaka 2025. (Bild, via Sun)
Arsenal wanamuwania kiungo mfaransa, Nabil Fekir kutoka Real Betis, lakini ofa ya washika bunduki hao haifikii kiwango wanachohitaji klabu hiyo ya La Liga kwa ajili ya nyota huyo mwenye umri wa miaka 27. (AS - in Spanish
Crystal Palace inajiandaa kupeleka ofa ya £15 kwa ajili ya kiungo wa kiingereza Conor Gallagher (21) kutoka Chelsea, ambaye anataka kusalia Stamford Bridge baada ya msimu uliopita kuonyesha kiwango kizuri akiwa West Brom kwa mkopo. (Sun)
West Ham, Southampton na AC Milan zinapambana kumsajili mlinzi wa Barcelona Junior Firpo, (24) raia wa Dominica, huku klabu hiyo ya Catalan ikigoma kumuuza kwenye klabu za ligi kuu England, badala yake ikitaka kumpeleka Milan kwa mkopo pakiwa na fursa ya kumsajili baadae moja kwa moja. (Mundo Deportivo - in Spanish)
Kiungo wa England, Jesse Lingard, 28, ameimwmabia meneja wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer kwamba anataka kusalia kwa mashetani hao wekundu, baada ya kuwa na wakati mzuri msimu uliopita aikiwa na West Ham kwa mkopo. (Sun)
Mlinda mlango wa Juventus, aliyenyakuwa pia kombe la dunia akiwa na Italia, Gianluigi Buffon, 43, anajiandaa kurejea Parma, ya Serea B, ikiwa ni miaka 20 tangu aondoke kwenye klabu hiyo. (Sky Italia - in Italian)
Meneja wa Norwich City Daniel Farke anataka kumsajili kiungo wa Bournemouth raia wa Denmark, Philip Billing (25), ambaye anataka kuondoka baada ya kabu hiyo kushindwa kupanda daraja kucheza ligi kuu ya England. (Mirror)
Kiungo wa Bernardo Silva (26) anataka kutimka Manchester City, huku vilabu vya Barcelona na Atletico Madrid vikionyesha nia ya kumtaka nyota huyo wa kimataifa wa Ureno. (Duncan Castles on Twitter)
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.