Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kwa wale wote wanaosumbuliwa na mba na miwasho, tangawizi ni ‘dawa’ nzuri kwa kulinda ngozi yako kwa kuwa ni anti-fungal ya kiasili, anti-septic na pia anti-inflammatory inayozuia matatizo na maradhi yoyote yale ambayo yanaweza kushambulia ngozi yako.
 
Heri jirani apewe kuliko kioze [emoji870][emoji870][emoji870]
IMG-20210618-WA0126.jpg
 
Namna ya kutumia tangawizi kwenye nywele

Toa maganda ya juu ya tangawizi.

Iponde halafu kamua maji yake.

Hayo maji yake unaweza kuyachanganya na asali au parachichi au Aloe vera.

Tangawizi isiwe nyingi; chukua kiasi kidogo tu.

Baada ya hapo, unapaka kuanzia chini kupanda juu na huku ukimasaji ngozi yako.

Halafu funika nywele zako kwa kitambaa kwa muda wa saa moja.

Baada ya hapo, osha ukitumia maji mengi.

Baada ya kuosha utapaka leave in conditioner.
 
Huondoa mwilini baadhi ya magonjwa au hali mbaya za kiafya

Tangawizi hupunguza na kuondoa kabisa hali mbaya za kiafya kama kikohozi na mafua. Tangawizi pia husaidia kuondosha uchovu hasa asubuhi.

Kwa akina mama wajawazito, tangawizi huwapunguzia homa za asubuhi pindi wanapoamka; na vilevile hutumika kama kichocheo cha utulivu.
 
Mshubiri (Aloe vera)

Mshubiri huwa na virutubisho muhimu vinavyohitajika kwa ngozi yako. Utahitaji jani moja la Aloe vera. Chukua Aloe vera kisha kata jani lake vipande vipande utoe jeli yake kisha upake kwenye lips. Unaweza kulala nayo. Tumia hadi uone matokeo.Tahadhari: Aloe vera ni chungu, kuwa muangalifu unapoitumia.
Jamani jamani
 
Back
Top Bottom