Brokoli ni mboga ambayo ina faida sana kwenye ubongo kwani ina vitamini K, C na inatoa kinga ya mwili. Vitamini K inahusika na utendaji kazi mzuri wa ubongo.
Mayai ya kuku, yana kirutubisho aina ya Choline. Kirutubisho hiki huzalishwa mwilini kwa kiwango kidogo tu, hivyo kwa kula mayai (ya kienyeji) utaweza kuongeza, kiwango cha kirutubisho hicho mwilini kwa kiwango kikubwa na hivyo kuimarisha afya ya ubongo.
Ubongo huongoza kufanya kazi na kusonga kwa viungo vya mwili, mawazo, kumbukumbu za akilini na kuhakikisha viungo vya mwili vinafanya kazi ipasavyo kwa uwiano na ushirikiano unaostahili.
Samaki huwa na virutubisho pamoja na mafuta ya Omega-3.Asilimia kubwa ya ubongo wa binadamu ni mafuta.Ubongo wa binadamu hutumia Omega-3 kutengeneza seli mpya. Mafuta hayo ni muhimu kwa kumwezesha mtu kujifunza kitu na kukumbuka.
Iwapo unakunywa kahawa asubuhi, utafurahia kusikia kuwa inafaa.Viungo viwili vya kahawa – kafeini na chembechembe za molekuli zinazosaidia kuzuia mchanganyo wa kemikali zinazoweza kuharibu seli za mwili, kwa kitaalamu anti-oxidants – vinasaidia ubongo wako.Pia kahawa inachangamsha na kuongeza viwango vya kemikali kwa jina serotonin inayomfanya mtu kujihisi akiwa na furaha.
Bizari manjano (Turmeric)Kiungo cha curcumin kinachopatikana kwa bizari manjano kimethibitishwa kufaidi seli za ubongo, kupunguza msongo wa mawazo na kuboresha uwezo wa kukumbuka.
Brokoli au Broccoli ina viungo muhimu vinavyosaidia kuondoa sumu mwilini. Aidha, mboga hii imesheheni vitamini K ambayo utafiti umeonyesha huchangia kuboresha uwezo wa kukumbuka.
Chokoleti ina viungo vya flavonoids ambavyo ni muhimu kuboresha eneo la ubongo linalohusika na kukumbuka au kumbukumbu.Pia ina viungo vya kafeini na vya kuzuia mchanganyo wa kemikali unaoweza kuziathiri seli, yaani anti-oxidants vinavyochangamsha ubongo.
Njugu zimesheheni vitamini E na vitamini za kundi la B ambazo ni muhimu kwa kuboresha afya ya ubongo.Vitamini E husadia ubongo wa mtu kuweza kuelewa lugha na mazungumzo pamoja na kumwezesha kuzungumza.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.