Rafael Benitez anakaribia kujiunga na Everton baada ya kufanya mazungumzo zaidi na klabu hiyo wikendi iliyopita, licha ya mashabiki kupinga mpango wa kuteuliwa kwa kocha huyo wa zamani wa Liverpool. (Mirror)
Crystal Palace wamefanya mazungumzo na Lucien Favre kuhusu uwezekano wa kuchukua nafasi ya Roy Hodgson lakini huenda wakakabiliwa na upinzani kutoka kwa Everton. (Guardian)
Mlinzi wa Ujerumani Antonio Rudiger, 28, anataka kusalia Chelsea msimu ujao ijapokuwa klabu hiyo haijaanzisha mazungumzo ya kurefusha mkataba wake wa sasa, ambao unakamilika msimu ujao. (Sky Sports)
Bayern Munich wameungana na Everton, AC Milan na Inter Milan katika mbio za kumsaka mchezaji wa kimataifa wa Uholanzi Denzel Dumfries,25, kutoka PSV Eindhoven. (Voetbal International - in Dutch)
Kiungo wa kati wa Lille na Ufaransa Boubakary Soumare, 22, atafanyiwa uchunguzi wa afya huko Leicester katika kipindi cha siku 10 zijazo kabla ya kusaini mkataba wa miaka mitano na klabu hiyo ya Ligi ya Premia. (La Voix des Sports - in French)
Liverpool hawana mpango wa kumuuza Kostas Tsimikas msimu huu wa joto licha ya mlinzi huyo wa Ugiriki aliye na umri wa miaka 25 kucheza mara saba pekee katika kikosi cha kwanza msimu uliopita. (Liverpool Echo
Roma wanajadiliana na Wolves kumhusu kipa wa Mreno Rui Patricio,33, kwa sababu klabu hiyo ya Ligi ya Premia inataka kumnunua kwa kati ya paundi milioni 10 na 13. (Sky Sports
Liverpool hawana mpanigo wa kumuuza Kostas Tsimikas msimu huu wa joto licha ya mlinzi huyo wa Ugiriki aliye na umri wa miaka 25 kucheza mara saba pekee katika kikosi cha kwanza msimu uliopita. (Liverpool Echo
Wolves wanataka kumsajili kipa wa Leicester na Wales Danny Ward, 27, ambaye ameonesha umahiri wake katika muchuano inayoendelea ya Euro 2020. (Football Insider)
Kocha wa Fulham Scott Parker anakaribia kusitisha mkataba wake na kiungo wa kati wa zamani wa England, kuchukua usukani baada ya hapo anatarajiwa katika klabu ya Bournemouth. (Sky Sports)
Mkuu wa wilaya ya Kisarawe Nikki wa pili akisikiliza hotuba fupi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani mh Abubakar Kunenge mara baada ya kuwaapisha wakuu wa wilaya za mkoa huo.