Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Walakini, kati ya wanawake wote maishani mwake, wale maarufu zaidi, labda, walioonyeshwa naye walikuwa walinzi wake wa kike waliozungumziwa sana. Jeshi lake la walinzi wanawake na timu za wauguzi wa kike zilimpatia umaarufu ulimwenguni.

Kulingana na ripoti, walinzi wake, pamoja na kuwa wanawake, walichaguliwa kwa kuwa mabikira. Kwa kuongezea, walipaswa kuchukua kiapo cha usafi na kuapa kuyatoa maisha yao kwa ajili yake. Inavyoonekana, walichukua viapo vyao kwa uzito - inasemekana hakuenda mbali naye mchana au usiku.
 
Walinzi hawa waliofunzwa walikuwa na ujuzi wa kijeshi na walikuwa wataalam katika utumiaji wa silaha, kulingana na ripoti mbali mbali za habari nje na ndani ya Libya. Jarida la Huffington lilisema wanawake hao walipata mafunzo mengi ya kijeshi na silaha katika chuo kikuu maalum kabla ya kuingizwa rasmi.
 
Walinzi wa Gaddafi walikuwa sawa na utawala wake. Angewatumia kama ishara ya imani yake katika ukombozi wa wanawake. Hata hivyo baadaye ufichuzi wa kutisha ulitolwa na baadhi ya wanawake waliokuwa katika kikosi hicho kwamba Gaddafi alikuwa akiwabaka na kuwafanyia unyanyasaji mwingine .
 
Ziara ya Gaddafi nchini Italia mnamo 2009 iligonga vichwa vya habari baada ya kutolewa mwaliko wa wasichana 500 wa kuvutia wa Italia kwa dhifa ya chakula cha jioni katika jumba ambamo Gaddafi alikuwa akilala .

Inasemekana alitumia hafla hiyo kuwashawishi wasichana hao wasilimu na akawapatia nakala ya kitabu chake cha Green Book.
 
Ripoti zilizoibuka baadaye zilidai kwamba walinzi hao wa zamani walisema Gaddafi na wanawe waliwabaka na kuwanyanyasa na kisha kuwatupa wanawake mara tu wanaume "walipokuwa wakichoka" nao.

Mwanasaikolojia aliyekuwa na makao yake katika mji wa Benghazi Seham Sergewa alikusanya maelezo ya kutumiwa na Korti ya Uhalifu ya Kimataifa (ICC), ambayo ilichunguza uhalifu wa kivita wa Gaddafi na washirika wake.
 
Mwendazake alikuwa na roho mbaya sana dhalimu. Bila Mwenyezi Mungu kumchukua Lissu asingelipwa haki zake za mamilioni ya shilingi
hapo ndipo huzaliwa tena tatizo la mfumo, watu wawili waliofanya kazi kwa pamoja wanatofautiana kifikra na maamuzi.
huyu ananyima stahiki za yule
huyu anarudisha stahiki za yule

ningelikuwa spika ningeliomba kupumzika (fedheha yamuangukia yeye)
tangazo hili latupa maana tusioijua, kumbe mihimili hii mitatu inamilikiwa na mtu mmoja tu.
RAISI​
 
Baada ya baadhi ya wanawake hao kujitokeza na madai kwamba waliakuwa wakibakwa ,wenzao kadhaa pia waliibuka na madai hayo .mtindo wa unyanyasaji wao ulikuwa ule ule.

Sergewa pia alichunguza madai kwamba wanajeshi wa Gaddafi walibaka wanawake wakati wa mzozo nchini humo uliosababisha kupinduliwa kwa serikali yake na kisha baadaye kuuawa .
 
Wanawake wengine walijitokeza wakisema walibakwa na wanajeshi 20 kwa wakati mmoja.

"Katika kisa kimoja, msichana, karibu miaka 18 au zaidi, alisema alibakwa mbele ya baba yake. Aliendelea kumwambia asimtazame, "Sergewa alisema.

Waathiriwa wengine wamejiua au walikuwa wakifikiria kujiua .
 
Mauaji ya Gadhafi

Wakati upepo wa uasi ulipoanza kuvuma katika ulimwengu wa Kiarabu kutoka Tunisia mnamo Desemba 2010, Libya haikuwa juu ya orodha ya watu wengi wa "nani afuataye".

Gaddafi kwa wengi alikuwa akionekana kama mtawala wa kimabavu ambaye alivumiliwa kwa miaka zaidi mingi kuliko idadi kubwa ya raia wake wanavyoweza kukumbuka. Lakini hakutambuliwa sana kama kibaraka wa magharibi kama viongozi wengine wa Kiarabu, walioshutumiwa kwa kuweka masilahi ya nje mbele ya maslahi ya watu wao wenyewe.
 
Kadiri maasi yalilivyoenea, na uzito wa tishio kwa utawala wake kuonekana, Gaddafi alionyesha kuwa hakuwa amepoteza unyama wowote ulioelekezwa dhidi ya wapinzani na waliotoroka nchi miaka ya 1970 na 1980.

Wakati huu miji mizima na vijiji vililengwa kwa ukatili wake ambapo watu walikuwa wamethubutu kurarua mabango yake na kutoa wito kumalizika kwa utawala wake . Wanajeshi wa kawaida na mamluki karibu wangewazidi nguvu waasi ambao hawakuwa na mafunzo ya kutosha , wakiwemo wanajeshi waliotoroka vikosi vya Gaddafi chini ya mwavuli wa Baraza la Mpito la Kitaifa (NTC).
 
Back
Top Bottom