Kwa kuacha kuvuta sigara utaweza kuokoa pesa ambazo huwa unazitumia kwa ajili ya kununua sigara, na kuzitumia kufanya mambo mengine yenye manufaa kwako.
Uvutaji wa sigara huathiri afya ya mwanadamu kwa namna mbalimbali. Hivyo kuacha kuvuta sigara kutakuepusha na maradhi kama vile shambulio la moyo, saratani ya mapafu, kuzeeka kwa ngozi, matatizo ya ubongo, n.k.
Ikiwa damu haitasafiri sawasawa, sehemu za mwili kama vile ubongo utakosa kiwango cha kutosha cha damu, jambo linaloweza kusababisha kiharusi na hatimaye kifo.
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na chuo Kikuu cha Washington mwaka 2007, unaeleza kuwa uvutaji wa sigara huchelewesha kwa kiasi kikubwa kupona majeraha ya vidonda.Hivyo hakuna haja ya kuvuruga mchakato wa wewe kupona majeraha kwa sababu ya kutumia sigara.
Sigara hukufanya kuwa mtawaliwa (addicted). Mara nyingi mtu anayevuta sigara hushindwa kujitawala, anaweza kuvuta hata usiku wa manane, hosipitalini, maeneo yenye mikusanyiko, n.k. bila kuweza kujizuia.Hivyo kuacha sigara hukufanya uweze kujitawala tena na si kutawaliwa na sigara.
Moshi wa sigara una zaidi ya kemikali 4,000 na 43 kati yake zinafahamika wazi kusababisha saratani za aina mbalimbali. Hivyo uvutaji wa sigara haukuathiri tu wewe bali hata wale wanaokuzunguka, hasa wanafamilia.Kuacha sigara kutalinda afya yako na wale wanaokuzunguka kwa ujumla.
Uchunguzi uliofanyika mwaka 2010 kwa watu wenye umri mkubwa ambao walikuwa wavutaji wa sigara, ulibaini kuwa walikabiliwa na matatizo ya akili kwa kiasi kikubwa ikilinganishwa na wale wasiovuta sigara.Kutokana na utafiti huu ni ukweli kuwa uvutaji wa sigara huathiri afya ya ubongo na hatimaye kupelekea matatizo ya akili.
Inaelezwa kuwa sigara huharibu mbegu za kiume, husababisha kutoka kwa mimba, huharibu mayai ya uzazi ya wanawake pamoja na kuathiri viungo vya uzazi kwa ujumla. Hivyo kuacha sigara ni kulinda afya yako ya uzazi.
Watu wanaovuta sigara wamekuwa wakiwakera watu wengi kutokana na harufu mbaya inayotokana na uvutaji wa sigara. Wengine wamekuwa wakitumia dawa mbalimbali ili kukabili harufu hiyo bila mafanikio.
Kwa hakika kuna kila sababu ya kuacha uvutaji wa sigara leo. Ikiwa unataka kuacha sigara inakupasa kufanya maamuzi sahihi pamoja na kuweka mikakati stahiki ya kufanya hivyo. Unaweza pia kutafuta msaada kutoka kwa wataalamu wa tiba au washauri nasaha ili kuweza kutimiza lengo lako
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.