Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

5. Kobe
Ndiye mnyama anayeishi miaka mingi duniani, pengine kuliko wanyama wengine wote hufikia miaka hadi 350, kwa Tanzania tunao wenye miaka 200+, kama nakuona raha za dunia zinavyokufanya utamani kuwa Kobe
 
6. Kicheche.
Ndiye mnyama anayependa ngono kuliko kiumbe yoyote, wanapokutana jinsia tofauti kabla ya salamu huanza kusasambua kwanza, yaani hawa katika jamii zao hata msibani hukutana kwa mapenzi pia, inakadiriwa kwa siku ili walale usingizini mwororo auheni wapitiane mara 60 na zaidi ! Na ndio sababu hata mtu akiwa kiwembe huitwa kicheche.
 
8. Tai
Ndio kiumbe mkorofi kupita kiasi ni kawaida kunyang'anya watalii chakula, ni kawaida kusumbua ndege wenzie wanapoatamia, kupigana nk ili mradi fujo.
 
9. Nyati
Mnyama mwenye hasira na kisasi kuliko wanyama wengine wote, simba wanamwelewa vyema sana huyu kiumbe, wakithubutu kuua mtoto wake na wao huenda kukanyaga watoto wake vile vile au vipi bwana jicho kwa jicho, jino kwa jino tuone sasa.
 
10. Kipepeo.
Ndiye kiumbe mpenda amani pasina mfano, ukipita msituni umenuna usitegemee watakusogelea, ila mkipita na mwenza wako, mnacheka mna furaha, ahaa utashangaa wanawapamba !
 
11. Simba.
Pengine sababu ya kuitwa Mfalme ni ubabe, Dume la simba ndio mnyama pekee anayejijua kwamba anaogopwa na hata majike wake wanapopata dhahama, akipata taarifa hujitokeza mara moja na ukiona madume yameongozana mawili basi jua huo mziki mwamuzi ni Mungu.
 
12. Mbu
Ndio kiumbe aliyeweza kuua binadamu wengi sana kuliko mnyama yoyote yule unayemfahamu wewe, utapokaona tafadhari Katie kitasa.
 
13. Komba
Ndiye mnyama mlevi kuliko wanyama wote na akilewa hulia pasina sababu ya msingi, hata ukibahatika kumuona sura yake imekaa kilevi levi, hupendelea pombe za kienyeji kuliko bia, we watege kwa mnazi au ulanzi sio misosi hapo utawapata.
 
15. Tembo
Ndiye mnyama mwenye uwezo wa kuhifadhi sana kumbukumbu katika kichwa chake, kama ulipojenga walihawi kupita tegemea kuna siku watakuwa wageni wako, wakati tunakazana kusema tembo wamevamia sehemu fulani tukae tukijua maeneo hayo wana historia nayo, sasa siku mpige jiwe mkutane baada ya miaka kumi ndio utajua ule mkonga ni bakora au pua.
 
Utafiti wa muda mrefu juu ya mnyama aina tembo umebaini baadhi ya tabia mabazo wanyama hawa wanzo zinafanana na zile ambazo binadamu anazifanya katika masiha yake ya kila siku.
 
Kuna aina mbili za Tembo, ambazo ni (Loxodonta Africana na Elephas maximus) Makala hii ya leo itazungumzia juu ya tabia hizo za tembo ambazo zinafanana na zile za binadam kama ifuatavyo;
 
Baada ya hapo tembo huingia hatua ya kubalehe ambayo hutofautiana kutoka jamii moja na nyingine na hata kati ya tembo mmoja na mwingine ndani ya familia, umri huo unakadiriwa kuanzia miaka 7 hadi17.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…