Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Baada ya kubalehe tembo huingia hatua ya ukomavu ambapo tembo dume huanza kusaka mwenza katika familia ambazo hawana mahusiano.
 
kwa mujibu wa taarifa za umoja wa mataifa za mwaka 2019 wastani wa umri wa binadamu kuishi ni miaka72.6 ambao uunashabiiana na ule wa Tembo.
 
Hivyo hivyo na tembo huishi katika mfumo wa familia ambao huundwa na tembo jike pamoja na tembo dume ambao hawajafikia umri wa kubalehe (ndama) wenye uhusiano wa karibu huku wakiongozwa na tembo jike mwenye umri mkubwa aitwaye Matriach kitaalamu.
 
tembo dume wafikishapo umri wa kubalehe, huondoka katika familia zao na wanaweza kuishi katika vikundi wakiwa na madume wengine au peke yao.
 
Hivyo basi tembo dume hulazimika kwenda kwenye familia nyingine na kutafuta mwenza ambaye huweza kuzaa pamoja.
 
Hii huthibitisha kuwa tembo wana uwezo mkubwa wa utambuzi kwani huwatambua ndugu zao na kuepuka mahusiano hata kama hajaonanana naye kwa muda mreufu.
 
Hili ni jambo la msingi katika ustawi wa wanyama hawa kwani huweza kupata watoto wenye mchanganyiko wa asili za familia tofauti ambao huwa na uwezo mkubwa wa kumudu mazingira yao.
 
Hekima hii ya tembo kuepuka mahusiano na ndugu haina tofauti na jamii nyingi za wanadamu ambapo ndugu kuoana au kuwa na mahusiano huwa ni mwiko.
 
Mazishi na kuomboleza
Tembo wawapo katika shughuli zao za kila siku huweza kutambua mifupa au mizoga ya tembo waliokufa ambapo husimama kwa muda na kufanya uchunguzi kwa kugusa mwili au mifupa kwa mkonge kisha huufunika (huzika) kwa nyasi au majani.
 
Back
Top Bottom