Vile vile migogoro kati ya binadamu na tembo nayo imefanya maisha ya wanyama hawa kuwa hatarini hususani pale wanapowaua kwa ajili ya kulipa kisasi pale tembo anapoharibu mazao.
Ulaji wa njegere mara kwa mara husaidia kuboresha kinga ya mwili, hurekebisha kiwango cha sukari kwenye damu lakini pia huzuia mtu kuzeeka kwa haraka na zina kiwango kidogo cha kalori.
Protini iliyopo katika mboga hii husaidia kuyeyusha damu iliyoganda na kwa wagonjwa wenye upungufu wa damu, wanatakiwa kutumia njegere zilizochemshwa kila siku.
Ulaji wa njegere za kijani huongeza damu, hukabiliana na udhaifu wa afya lakini zinasaidia kupunguza maumivu katika kidonda kinachouma kwa sababu inasaidia kuondoa asid zilizopo tumboni.
Utafiti uliofanywa na mtaalamu wa tiba-lishe wa taasisi moja nchini Marekani, Dk.George Mateljan anasema, njegere ni miongoni mwa vyakula vyenye kiwango kikubwa cha kamba lishe zenye uwezo wa kushusha kiwango cha lehemu inayosababisha shambulio la moyo.
Matokeo ya utafiti wake huo aliouandikia kitabu kiitwacho The World’s Healthiest Foods, Dk Mateljan anasema asilimia 65 ya mbegu ya njegere ni kamba lishe ambapo pamoja na kushusha lehemu, pia huondoa shinikizo ya damu na kuzuia shambulio la moyo. “Watu wengi wanakula kidogo sana, hawajui faida hizi.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.