Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Vivo hivo tembo huwa na mapenzi makubwa kwa mwana, humyonyesha kwa takribani miaka mitano na muda wote huo mama hujitoa kwa ajili ya kumtunza na kumlinda mtoto dhidi ya maadui.
 
Ingawa usalama wa mtoto tembo huwa ni jukumu la tembo jike wote katika familia, ila mama huonyesha kuguswa sana na mtoto wake mfano tembo wanapovuka barabara, mama husimama barabarani na kuhakikisha mtoto wake amevuka ndipo naye avuke
 
Kutokana na upendo wa mama na mtoto tembo mwenye mtoto huchukua tadhari sana na huwa tayari kupambana na kitu chochote kinachoweza kumkaribia au kumdhuru, hivyo haina budi kuchukua tahadhari kubwa unapomwona mwana tembo, usimkaribie ama kumchezea.
 
Kushirikiana wakati wa shida dhidi ya maadui wao
Kama ilivyo kwa binadamu kusaidiana na hata kuwapa faraja wale wenye matatizo, tembo pia huweza kuwatambua wenzao wasipokuwa na furaha na kuwapa ulinzi pamoja na faraja.
 
Tembo huonesha tabia nyingi za upendo na kujali kama vile kutoa uchafu au kitu chochote kilichojishikiza kwenye wimili wa tembo menzao
 
Tembo alipojitazama kwenye kioo aliweza kugundua alama hiyo usoni mwake na kuanza kuifuta kwa kutumia mkonge wake, hii inathibitisha kuwa tembo anaujua uso wake
 
Watafiti wameeleza kwamba tembo huweza kuwatambua majangili ambao waliwawinda au waliowauwa wenzao hata kwa miaka mingi iliyopita.
 
Husalimia ndugu
Tembo huwa na desturi ya kutembeleana na kuwajulia hali wanafamilia ambao wametengana.
 
Tabia hii imeonekana kwa tembo dume wanapoondoka kwenye familia huwa na tamaduni ya kuzitembelea familia zao za awali ili kuwasalimia.
 
Pia pale familia ya tembo inapotengana au kugawanyika kutokana na sababu mbalimbali mfano familia kubwa, migogoro na uhaba wa chakula tembo huendelea kudumisha undugu kwa kukutana mara kwa mara
 
Huwa na muda wa kustarehe
Binadamu huwa na desturi ya kutenga muda wa kustarehe kwa kufanya mambo mbalimbali vivo hivo kwa wanyama hawa hutenga muda pia wa kucheza na kufarahi.
 
Back
Top Bottom