Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Utafiti zaidi unahitaji kufanywa kuhusu athari za moto kwa mimea na wanyama fulani hususa. Utafiti zaidi unahitaji pia kufanywa kuhusu faida na athari za moto kwa viumbe na mazingira.
 
Siku hizi kuna programu za kompyuta zinazoigiza hali halisi za mazingira, ambazo zimebuniwa ili kutabiri hali ya moto. Programu hizo hufasiri vipimo vya joto, vitu vinavyochochea moto, mwendo wa upepo, na hali nyingine za hewa.
 
Lakini programu zilizopo sasa si sahihi nyakati zote, na haziwezi kutabiri matukio ya pekee kama mlipuko wa moto au kuongezeka ghafula kwa moto. Wazima-moto wawili wenye uzoefu waliteketea wakati moto wa msituni ulipolipuka ghafula huko Sydney mwaka wa 1997. Milipuko hiyo ya ghafula huwa hatari sana.
 
Pepo zinaweza kubadili mwelekeo au mwendo ghafula, basi inakuwa vigumu kuudhibiti moto huo. Watafiti wanatumaini kuboresha programu zilizopo kwa kuongeza habari nyingine kama vile mwinamo na umbo la ardhi na kiasi cha vitu vinavyochochea moto.
 
Kituo cha Kitaifa cha Utafiti wa Hali ya Hewa (NCAR) huko Colorado, Marekani, kinajitahidi kufikia lengo hilo. Watafiti hao wametia vifaa vya kisasa vya kisayansi pamoja na kompyuta saba zilizohifadhiwa kwenye vifuniko vizito ndani ya ndege maalumu aina ya C-130.
 
Ndege hiyo imebuniwa ili iweze kupaa juu ya moto unaoenea na kukusanya habari fulani kwa kutumia vifaa maalumu vilivyo kwenye mabawa yake. Habari hizo huingizwa kwenye kompyuta ili zichunguzwe. Ndege hiyo ina kamera inayoitwa Thermacam inayotumia miale isiyoonekana ambayo inaweza kuonyesha ukali wa kila sehemu ya moto. Kwa njia hiyo wanasayansi wa NCAR wanajifunza kuboresha programu zinazopima hali ya moto.
 
Back
Top Bottom