Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Wakulima wanapotumia moto kwa njia nzuri, wanaboresha ardhi kama mioto ya asili inavyofanya. Hata hivyo, mbinu ya kale ya kukata na kuteketeza vichaka kwa ajili ya kilimo imeenea sana siku hizi.
 
Njia rahisi na isiyogharimu ya kutayarisha ardhi ni kuteketeza misitu. Kwa hiyo, watu huteketeza maeneo yenye ukubwa wa maelfu ya eka bila kujali faida za muda mrefu za kuhifadhi misitu.
 
Faida za Moto

Ijapokuwa moto unaweza kusababisha uharibifu mkubwa sana na hasara, unaweza pia kufaidi mimea mingi na wanyama wengi. Kwa kweli, moto unaweza kuboresha mazingira. Namna gani?
 
Makabila ya asili ya Australia yametumia moto kwa mamia ya miaka katika shughuli mbalimbali za kila siku. Kabila la Yanyuwa linathamini sana moto hivi kwamba lina zaidi ya majina kumi na mbili kwa ajili ya mioto mbalimbali na athari zake. Kwa mfano, wao huuita moto wa vichakani au wa porini kambambarra. Sehemu iliyoteketezwa na inayofaa uwindaji huitwa warrman. Moshi unaopaa angani na kufanyiza wingu huitwa rrumarri.
 
Wakazi hao wa asili huteketeza vichaka ili mimea mipya ichipuke. Wao hutumia mioto midogo kuteketeza majani makavu yaliyorundamana mashambani, ambayo mara nyingi huchochea mioto ya misitu. Kutumia moto kwa njia hiyo kumewawezesha wakazi wa asili wa Australia wajiruzuku kwa kilimo huku wakihifadhi misitu na wanyama. Kumepunguza pia hatari ya watu kuteketezwa na mioto hatari ya misitu.
 
Umuhimu wa Kudhibiti Moto

Wazungu walipowasili Australia zaidi ya miaka 200 hivi iliyopita, walianza kuvuruga uhusiano kati ya wanadamu, mazingira, na moto.
 
Kwa maoni ya Wazungu, mioto ya misitu ilihitaji kukomeshwa. Kwa hiyo visa vya moto vilipungua, lakini kwa sababu majani makavu na vijiti viliongezeka, mioto iliyozuka ilikuwa mikali zaidi na haikuzimika kwa urahisi.
 
Hata hivyo, hivi karibuni serikali zimeona umuhimu wa mbinu za wakazi wa asili wa Australia na wameanzisha mbinu ya kuteketeza majani ya msituni kwa mpango. Kwa kutumia mbinu hiyo moto hudhibitiwa ili usisababishe hasara.
 
Mioto midogo huwashwa kabla ya majira ya kiangazi. Mioto hiyo husambaa polepole, si mikali sana, na huteketeza majani yote bila kuharibu miti. Kwa kawaida, umande huzima mioto hiyo wakati wa jioni.
 
Mioto midogo huwashwa kabla ya majira ya kiangazi. Mioto hiyo husambaa polepole, si mikali sana, na huteketeza majani yote bila kuharibu miti. Kwa kawaida, umande huzima mioto hiyo wakati wa jioni.
 
Yaonekana mbegu za mimea fulani hutegemea moto ili ziote. Baadhi ya mbegu hizo zina maganda magumu sana ambayo yanahitaji kuteketezwa na moto kuwezesha unyevunyevu upenye ndani.
 
Utafiti unaonyesha kwamba moshi unasaidia pia mbegu kuota. Yadhaniwa kwamba moshi una kemikali 70 hivi ambazo zinachangia ukuzi wa mbegu. Kemikali moja muhimu ni nitrojeni-dioksidi.
 
Moto hutokeza virutubishi kutokana na majani, huruhusu mwangaza wa jua kupenya ardhini, na huboresha ardhi ili miche isitawi. Kwa mfano, mbegu za migunga, huchipuka baada ya kuteketezwa na moto na miti hiyo husitawi katika mazingira hayo.
 
Jamii fulani za kangaruu na wallaby hupendelea misitu inayoteketezwa mara kwa mara. Yasemekana kwamba wanyama hao wanategemea moto kwa sababu mimea wanayokula na mahali wanakoishi husitawi sana baada ya kuteketezwa.
 
Back
Top Bottom