Mmiliki wa Chelsea Roman Abramovich anayekabiliwa na vikwazo vya serikali ya Uingereza ameipatia Manchester United nafasi ya kumsajili mkufunzi wa The Blues Thomas Tuchel, kwa mujibu wa beki wa zamani wa Liverpool na Uingereza Jamie Carragher. (Telegraph - usajili unahitajika)
Chelsea ina wachezaji tisa ambao mikataba yao inamalizika msimu huu wa joto na huenda wakaondoka bila malipo kufuatia hatua ya serikali ya Uingereza kumwekea vikwazo Mrusi Abramovich. (Metro)
Mkataba wa beki wa Ujereumani Antonio Rudiger katika klabu ya Chelsea unamalizika msimu huu wa joto na mchezaji huyo wa miaka 29 anajiandaa kuondoka baada ya the Blues kukosa nafasi kadhaa za kumpatia mkataba mpya (Sky Sports News, via Star)
Juventus wanatafakari uwezekano wa kumnunua mshambuliaji wa Chelsea na Marekani Christian Pulisic, 23 msimu huu wa joto. (Gazetta dello Sport - kwa Kitaliano)
Manchester United wanapanga kuanza mazungumzo na mlinzi wa Ureno Diogo Dalot kuhusu mkataba mpya, huku mchezaji huyo wa miaka 22 akisalia na miezi 18 katika mkataba wake wa sasa. (Teamtalk)
Valencia wanataka kusalia na winga wa Tottenham Bryan Gil, 21, kwa mkopo msimu ujao na huenda wakamuongeza mwaka mmoja Mhispania huyo katika mkataba w wake wa mkopo. (Star)
Brighton wanaonekana kuongoza mbio za kumsaka mshambuliaji wa Blackburn Rovers Ben Brereton Diaz, huku Crystal Palace, Everton, Leeds United na West Ham pia zikimtaka kiungo huyo wa kimataifa wa Chile mwenye umri wa miaka 22. (Teamtalk)
Mwaka 2019 Rashford alisaini mkataba wa United wa kulipwa £200,000-kwa wiki unaoishia June 2023 lakini amekua na kiwango kibovu msimu huu. (Manchester Evening News)
Mshambuliaji wa United mreno Cristiano Ronaldo, 37, anajiandaa kusalia Manchester United msimu ujao, huku meneja wa muda Ralf Rangnick akitarajiwa kuondoka. (AS)
Arsenal wanataka kumsajili mshambuliaji wa zamani wa Chelsea aliyeko Real Madrid Eden Hazard, 31. Mbelgiji huyo alijiunga Real mwaka 2019. (FootMercato - in French)
Benfica imemuwekea bei ya £67m mshambuliaji wake raia wa Uruguay Darwin Nunez, 22, ambaye aliisaidia klabu hiyo ya Ureno kufika robo fainali ya ligi ya mabingwa Ulaya. Nunez anavivutia pia vilabu vya Arsenal, Manchester United naNewcastle. (Mirror)