Yeyote anayesafiri umbali wa zaidi ya maili 48 (kilomita 80) pia ameruhusiwa kula, lakini lazima alipe saumu baadaye, kwa hivyo hii inajumuisha wachezaji wanaoenda kwenye michezo ya ugenini.
Muslim Chaplains in Sport (MCS) ilianzishwa mwaka wa 2014 na ndilo shirika pekee la aina yake kuidhinishwa na kufadhiliwa na Premier League na EFL, likifanya kazi katika vilabu vyote 92 vya taaluma ya kandanda kutoa mihadhara na semina za elimu.
Vilabu vya Ligi Kuu ya Uingereza mara kwa mara hutafuta mwongozo wa Kiislamu kutoka kwa MCS kwa niaba ya wachezaji wao Waislamu, ikiwa ni pamoja na masuala kama vile kuahirisha mifungo ili uchezaji wao wa mazoezi na wakati wa mechi usiathiriwe.
Ingawa hakuna uamuzi wa Kiislamu kwa wanariadha, tunatoa ushauri kuhusu jinsi wanavyoweza kudumisha imani zao na kujadili kama wanafuzu kusamehewa, kama vile wanapokuwa safarini au wagonjwa," mkurugenzi mkuu wa MCS Ismail Bhamji aliambia BBC Sport.
Klabu moja ya Ligi Kuu iliniomba nizungumze na mchezaji Mwislamu ili kuahirisha mfungo wake wa Ramadhani. Kiislam hana sifa kwa sababu masharti fulani yaliyotajwa lazima yatimizwe na lazima niwe muwazi na mkweli kwao juu ya ukweli mbaya."
MCS inafanya kazi kwa karibu na klabu mbili kuu nchini, Manchester City na Liverpool, na Bhamji alitoa hotuba ya Ramadhani katika Kampasi ya Etihad siku ya Jumatano, huku pia akisifu mbinu zao za utofauti na kupanua ujuzi wao kuhusu masuala haya.
City na Liverpool zinafanya vizuri zaidi na ninaona misingi iliyowekwa kwenye klabu hiz mbili," alisema. "Kuanzia chuo cha mafunzo na kuendelea, wana watu sahihi na wenye fikra sahihi na maono ya kusaidia klabu hadi kwenye kikosi cha kwanza.
Makocha] Pep Guardiola na Jurgen Klopp wanasifika kwa sababu wana maendeleo na wanafikiria mbele kwa hivyo nimeona maboresho yakifanywa katika kllabu kwa misimu kadhaa."