Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Paris St-Germain wanahusishwa katika mazungumzo ya kusaini mkataba na mshambuliaji wa Chelsea Romelu Lukaku mwaka mmoja tu baada ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Ubelgiji mwenye umri wa miaka 28 kuwagharimu Blues pauni milioni 98 kutoka Inter Milan. (But via Sun)
 
Manchester United na Arsenal wamejiunga na mbio za kumshaka Darwin Nunez baada ya kutuma ujumbe wake kumfuatilia mshambuliaji wa Uruguay mwenye umri wa miaka 22 wikendi ambaye kwa sasa anachezea klabu ya Benfica. (Mirror)
 
Roma, AC Milan na Juventus wamejiunga na West Ham pamoja na Newcastle katika kuelezea nia yao ya kusaini mshambuliaji wa Jesse Lingard, 29, wakati mkataba wake katika Manchester United utakapomalizika msimu huu. (Mirror)
 
Manchester United wanapanga kukamilisha kupanga safu yao ya kati msimu huu, huku kiungo wa kati Mfaransa mwenye umri wa miaka 29 Paul pogba alitarajiwa kuondoka wakati mkataba wake utakapoisha mwezi Juni mwaka huu. (Mirror)
 
Fursa za Tottenham za kusaini mkataba na mlinzi Mcroatia Josko Gvardiol msimu huu "huenda zisifanikiwa kabisa" huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 akisema anafurahia kuwepo katika klabu ya Ujerumani ya RB Leipzig. (RB Live - in German)
 
Klabu kadhaa za Primia Ligi na Ulaya zinatarajiwa kuchukua hatua ya kumchukua mlinzi Muingereza anayechezea klabu ya Chelsea- Levi Colwill mwenye umri wa miaka 19, ambaye anacheza mchezo wa kufurahisha akiwa na mkataba wa mkopo hatika Huddersfield msimu huu. (Fabrizio Romano)
 
Chelsea wamewasiliana na mshambuliaji wa chuo cha Arsenal cha Khayon Muingereza Edwards juu ya uwezekano wa uhamisho, huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 18 akiwa bado hajaamua mkataba wa kikazi na Gunners. (Goal)
 
Mshambuliaji wa Uhispania Marco Asensio anatarajia kuondoka Real Madrid msimu huu huku AC Milan na Tottenham wakiwa na nia na kijana huyo mwenye umri wa miaka 26 . (Mundo Deportivo - in Spanish)
 
Mshambuliaji wa Liverpool Mmisri Mohamed Salah anasema sio muda unafaa kuzungumzia kuhusu mazungumzo ya mkataba wake yanayoendelea na klabu yake, ambayo mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 ameyaeleza kama "hali ya siri". (Sky Sports)
 
Barcelona ainamini winga Mfaransa mwenye umri wa miaka 24, Ousmane Dembele, ambaye atakuwa huru katika msimu wa kiangazi, atajiunga na Paris St-Germain kama mshambuliaji Kylian Mbappe, 23, ataondoka katika klabu hiyo ya Ufaransa. (El Nacional - in Catalan)
 
Back
Top Bottom