Miongoni mwa rafiki wachache tulionao porini (mbugani) ni pamoja na ndege huyu Mwenzi wa asali, mwenye uwezo mkubwa wa kusikia sauti ya binadamu ikimuita na kuitii.
Pamoja na uwezo mkubwa Mwenyezi Mungu aliotujalia wa kufikiria na utimamu mkubwa wa akili bado binadamu tunauwezo mdogo wa kuamini kila kitu, hivyo kumechangia binadamu kuwa na marafiki wachache sana porini (mbugani) hasa kwa hawa viumbe pori.
Baadhi ya marafiki hao wachache tulionao ni kama ndege huyu Mwenzi wa asali, Mnandi ambae amekuwa akitumiwa na wavuvi wa asili hasa katika tamaduni za Japani na China ambapo huongozana moja kwa moja mpaka kwenye kina chenye samaki wengi hivyo baada ya kuvua samaki hugawana;
Tukirudi kwa rafiki yetu huyu mkubwa ndege Mwenzi wa asali, katika upangaji na uchambuzi wa kibiologia wanaelekeana na ndege waimbao (order Passeriforms
Ndege huyu Mwenzi wa asali katika jamii yao wametawanyika sana maeneo ya kitropiki ya bara la Afrika, Asia na Ulaya ikiwa upande wa Afrika tumejaliwa spishi nyingi na spishi mbili tu kuwepo barani Asia
Ndege huyu ana umbile dogo kati ya inchi 4.5-8 lillilopambwa na rangi nyeusi ya kupooza (kupauka) na njano inayongaa sana kwenye bega karibu na mbawa, rangi nyingine nyeupe kwenye mkia wake na rangi ya pinki kwenye midomo yake hii ni kwa spishi zote zinazopatikana barani Afrika.
Uwezo wao wa kula asali umechangiwa na ngozi nene ya miili yao isiyopitisha miiba ya nyuki na pia mfumo wao wa umengejaji ambao upo kwa jamii chache za ndege ambao unaweza kumengenya masega ya asali kutokana na bakteria waliomo ndani yao wasiopatikana kwa ndege wengi.
Uzalianaji wa ndege huyu Mwenzi wa asali;Ni miongoni mwa ndege wanaotaga kwenye viota vinavyotumika na ndege wa jamii nyingine kabisa hasa viota vya white eyes na warblers, Na viota hivi vingi vipo chini ya ardhi sana sana kwa jamii za ndege wanaokula nyuki.
Ndege huyu Mwenzi wa asali hutaga mayai matano kwa kipindi cha siku tano hadi siku saba na ndege huyu jike huhakikisha vifaranga vyake huatamika mwanzoni kwa sababu wanauwezo mkubwa wa kuanza kuyaatamia mayai yao kabla ya kutaga,
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.