Kwa kila mara unazama kwenye penzi zito (fall in love) wastani unapoteza marafiki zako wawili wa karibu. Hiyo ni kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu Cha Oxford.
Black-footed Cat ndio jamii ya Paka hatari zaidi kuliko wote, Wanapatikana katika vichaka vidogo na huwinda usiku tu. Kwa usiku mmoja anaweza kuua zaidi ya wanyama 14 tofauti tofauti, Huua kuanzia ndege mpaka wanyama wengine wadogo wadogo. Kwa kila windo analowinda ni nadra kukosa.
Kabla ya Thomas Edison kugundua taa ya umeme mwaka 1879, inaelezwa kua watu wengi kwa wastani usiku walikua wanatumia saa 10 kwa kulala tu (walikua wanalala mapema zaidi).
Robert G Heft, akiwa na umri wa miaka 17 mwaka 1958, alibuni bendera ya Marekani inayotumika sasa hivi. Ubunifu huo ulikua ni sehemu ya kazi za mikono kwenye somo la stadi za kazi shuleni. Alipata "B- (hasi)", lakini baada ya bendera hiyo kupitishwa kuwa bendera ya nchi, 1960, mwalimu wake alimuongezea maksi akampa "A".
Homoni ya Testosterone' kwa wanaume kwa kawaida huwa juu zaidi kwa asubuhi na hushuka usiku, kitendo hicho huweza kumfanya mtu kua mchovu, hamu, ongezeko la hisia n.k