Umewahi kusikia waswahili wakisema kuwa "una Bahati ya Ngekewa?", Basi buana leo nakuletea habari ya Ngekewa mwenyewe na bahati yake aliyopewa toka kwa Muumba wake.
Ngekewa ni mnyama jamii ya Panya (rodent) mwenye umbo na muonekano unaoshabiriana na mchanganyiko wa Nguruwe kimaumbile lakini anakuwa na Sura kama ya Panya.
Maajabu ya mnyama huyu yanawaacha hoi wanasayansi waliobobea kwenye taaluma ya wanyama kwani ni myama anayeongoza kwa kupendwa zaidi na kila aina ya kundi la.wanyama kuanzia; ndege, mamba, samaki, simba, kobe, nyoka na wadudu.
Inasemekana kuwa mnyama huyu hapigi kelele, hakimbii ovyo wala hatembei kwa haraka na vishindo, Pia mara nyingi anapohisi uchovu, basi huamua kuajilaza chini au kuondoka zake bila kuwabughudhi wanyama wengine waliojuu na pembeni yake.