Chelsea wanajiandaa kumuacha Mshambuliaji wao Mbelgiji Romelu Lukaku aondoke katika klabu hiyo msimu huu , huku Inter Milan na Paris St-Germain zakimtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28. (90 Min)
Manchester United wameweka bei ya pauni milioni 40 kama bei ya mlinda lango wa England Dean Henderson, 25, ambaye yuko makini kuondoka Old ttraford msimu huu, huku Newcastleikiwa ni miongoni mwa klabu zinazomlenga. (Star)
Meneja ajaye wa Manchester United Erik ten Hag atamleta msaidizi wake wa Ajax Mitchell van der Gaag pamoja naye katika Old Trafford lakini Robin van Persie bado hajaamua juu ya ofay a kumtaka ajiunge na kikosi cha wakufunzi katika klabu hiyo. (Mirror)
Roma wanaangalia uwezekano wa kumuachilia kiungo wa kati Nicolo Zaniolo aondoke mwishoni mwa msimu na wataangalia uwezekano wa ofa ya euro zipatazo milioni 60 (£49.6m) huku klabu za Serie A na Primia Ligi zikimtaka mchezaji huyo . (Corriere dello Sport - in Italian)
Liverpool wanamfukuzia kiungo wa nyuma-kulia wa klabu ya Aberdeen Mskochi Calvin Ramsay na wanamtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 18 kukaba nafasi ya Trent Alexander-Arnold. (Sun)
Kiungo wa kati wa Brentford Mjerumani Vitaly Janelt, 23, anasema amekuwa na mawasiliano kutoka klabu za primia Ligi na Bundesliga juu ya uwezekano wa kuhama baada ya kucheza vyema katika Nyuki hao msimu huu. (Kicker)