Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Huwa na radha tamu na harufu ya kuvutia zaidi, unatoka katika nchi ya Sri Lanka katika mmea ujulikanao kama Cinnamon Zeylanicum. Hujulikana pia kama mdalasini wa India.
Huwa na rangi ya kahawia (light brown), mwembamba na mlaini.
 
Cassia cinnamon
Wakati ule ambao ni feki na ni sumu pia hujulikana kama ‘Cassia cinnamon’ ni mdalasini huu ambao katika baadhi ya nchi umepigwa marufuku kutumika wala kuingizwa nchini mwao. Hujulikana pia kama mdalasini wa China na wengine huuitwa Saigon.
 
Mdalasini huu unatoka katika nchi za China, Vietnam na Indonesia. Wenyewe huwa una joto zaidi na huwa na radha kali na ya kuwasha ukiutumia. Madhara yake ni pamoja na kudhuru Ini na figo ukitumika kwa kipindi kirefu.
 
Kwa kawaida ni vigumu kutofautisha aina hizi mbili za mdalasini ukishakuwa tayari katika mfumo wa unga tofauti na ukiwa bado katika fimbo au magome. Mhimu ni ununuwe kutoka kwa mtu unayemuamini zaidi.
 
Kwa kawaida ni vigumu kutofautisha aina hizi mbili za mdalasini ukishakuwa tayari katika mfumo wa unga tofauti na ukiwa bado katika fimbo au magome. Mhimu ni ununuwe kutoka kwa mtu unayemuamini zaidi.
 
ANGALIZO KUHUSU ASALI FEKI:
Napenda kukufahamisha kuwa miaka ya karibuni kumejitokeza baadhi ya wafanyabiashara kutengeneza asali feki kwa kutumia maji ya miwa na sukari guru au kuongeza maji na vimiminika vingine ndani ya asali ili wajipatie faida kubwa, endapo utatumia asali ya namna hii basi utakuwa ukiihatarisha afya ya mwili zaidi badala ya kujitibu.
 
Zifuatazo ni mbinu za kuitambua asali ambayo ni salama kwa maana ya kwamba haijachakachuliwa:


* Weka maji kwenye glasi na kisha mimina asali ndani yake na kwamba ikikaa chini ya glasi bila kuchanganyana na maji basi hiyo ni asali asilia na inakuwa haijachanganywa na chochote.
 
Njia ya pili ni kuiweka asali kwenye njiti ya kiberiti na kisha kuiwasha hiyo njiti ya kiberiti, ikiwa njiti hiyo itawaka basi asali haijachakachuliwa kwa kuchanganywa na chochote lakini njiti ya kiberiti isipowaka asali hiyo inakuwa ni feki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…