Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

IMG_9681.jpg
 
Ipo tofauti kubwa kati ya mtu anayefanya au kutekeleza mradi wake akiwa na mpango na yule ambaye anafanya shughuli zake bila kuwa na mpango wowote.Watu hawa watatofautishwa na matokeo au matunda.
 
Watu wengi wameshindwa kuwa na matokeo makubwa katika mambo mengi wanayofanya si kwa sababu labda mambo wanayofanya siyo mazurii! Hapana ni kwa sababu tu hawana mpango wowote unaowaongoza kufanya yale wanayofanya.
 
Ni kweli unaweza kuishi bila kuwa na mpango wowote kama walivyo watu wengi na maisha yakaendelea lakini hutapata matokeo makubwa maishani mwako na itakuwa vigumu sana kuliishi kusudi la kuwepo kwako duniani.
 
Kwa kuwa kila binadamu ameumbwa ndani mwake akiwa amebeba kusudi maalum la kuishi kwake, ni vigumu sana kuliishi kusudi kikamilifu kufaulu katika dunia hii yenye msongamano wa mambo na shughuli nyingi.
 
MPANGO NI NINI?

Kwa lugha rahisi mpango ni hatua ya kutafsiri ndoto au maono kutoka kuwa katika namna ya wazo na kuliweka katika karatasi. Ni hatua ya kumaliza hata kabla ya kuanza. Mpango unabeba kusudi na kuonyesha njia ya namna ya kulifikia hilo kusudi.
 
Napenda sana hii tafsiri ya hayati mchungaji Dr Myles Munroe anaposema nanukuu “Planning is applying purpose to time. Time is present anyhow, planning is giving that time meaning or purpose. Planning is giving meaning to unused time.
 
Kupanga ni kuliweka kusudi kwenye muda,muda upo kwa namna yoyote. Kupanga ni kuupa maana au kusudi huo muda. Ni kuupa maana muda ambao haujatumika” mwisho wa kunukuu.
 
Kubadilika ni mojawapo ya sifa muhimu za mpango. Mpango unaweza kufanyiwa mabadiliko kisichobadilika ni kusudi lakini mpango unaweza kubadilika kwa sababu moja au nyingine. Sasa huwezi kufanyia mabadiliko mpango kama huna huo mpango.
 
Mpango ni hatua ya kwanza ya utekelezaji wa mradi au biashara yoyote ambayo inatarajiwa. Watu wengi wanakuwa na mawazo na kukurupuka kuanza kutekekeleza bila kuwa na mwelekeo matokeo yake wanaishia njiani.
 
FAIDA ZA KUWA NA MPANGO

Zipo faida nyingi za mtu,biashara au kampuni ikiwa na mpango ukilinganisha na mtu asiyekuwa na mpango kabisa.Zipo nyingi lakini leo nataka kukushirikisha chache tu ili uone umuhimu wa kuwa na hiki kitu.
 
Back
Top Bottom