Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Ili kusisitiza umuhimu wa mpango katika maisha leo nataka kukushirikisha faida ambazo mtu au kampuni yenye mpango itazipata ikilinganishwa na mtu ambaye yeye hana kabisa mpango lakini anaishi
 
KUKUONYESHA UNAKOKWEDA (KUSUDI)

Kabla mtu au kampuni haijafikria kuandika au kumpa mtu kazi ya kuandika mpango wake;ni muhimu kuwepo na kusudi bayana la kampuni,huduma au biashara inayotaka kuanzishwa. Kama kusudi halijajulikana ni vigumu sana mpango kukamilika
 
KUKUONYESHA UNAKOKWEDA (KUSUDI)

Kabla mtu au kampuni haijafikria kuandika au kumpa mtu kazi ya kuandika mpango wake;ni muhimu kuwepo na kusudi bayana la kampuni,huduma au biashara inayotaka kuanzishwa. Kama kusudi halijajulikana ni vigumu sana mpango kukamilika
 
Katika dunia hii yenye shughuli nyingi tunayoishi ni rahisi sana kufikiri kuwa unaweza kushiriki katika kila fursa itakayokuja mbele yako. Kujua kusudi la kuwepo kwako na kuliishi itakusaidia sana kujielekeza kwenye shughuli ambazo zitapelekea kutekeleza kusudi la kuwepo kwako.
 
Mpango unasaidia sana mtu kuweza kujielekeza kwenye shughuli moja ambayo ni muhimu katika maisha yake kwa kuwa unalo kusudi la maisha hivyo unajua unakoelekea. Hutapelekwa na upepo wowote unaoweza kuvuma.
 
HUONYESHA NJIA YA KUFIKA HUKO

Faida nyingine kubwa ya mpango unakuonyesha njia na namna ya kufika kule unakotaka kufika au kwenye kusudi lako. Inakupa njia sahihi ya kuweza kukufikisha kule unakotamani kufika kulingana na mpango wako.
 
Ukiwa na mpango huwezi kuenda vyovyote kwa kubahatisha tu. Hapa siongelei habari ya kuwepo uwezekano wa kuondokana na changamoto ya aina yoyote katika kipindi chote cha itekelezaji la! Pamoja na changamoto utakazokutana nazo njia ya kufika unakotaka kufika inabaisnishwa vizuri na mpango.
 
KUONYESHA VIKWAZO NA FURSA ZILIZOPO

Faida nyingine ya kuwa na mpango ni kukuonyesha nguvu (fursa) na udhaifu (vikwazo) vililivyopo vyote vikiwa na maana ya kukusaidia kufika kule unakotaka kufika.Kujua nguvu uliyo nayo na vikwazo vinavyoweza kukuzuia kufika kule unakotaka kufika ni jambo muhimu sana katika maisha.
 
KUONYESHA VIKWAZO NA FURSA ZILIZOPO

Faida nyingine ya kuwa na mpango ni kukuonyesha nguvu (fursa) na udhaifu (vikwazo) vililivyopo vyote vikiwa na maana ya kukusaidia kufika kule unakotaka kufika.Kujua nguvu uliyo nayo na vikwazo vinavyoweza kukuzuia kufika kule unakotaka kufika ni jambo muhimu sana katika maisha.
 
Haitatosha tu kujua lakini fursa na nguvu uliyonayo itakusaidia kuitumia kikamilifu kutimiza kusudi la kuwepo kwako duniani na udhaifu na vikwazo unavyoviona ni chachu kukuwezesha kuviondoa na kuweka njia sahihi ya kuvidhibiti.
 
KUBAINISHA MAHITAJI.

Hakuna shughuli,huduma,mradi au biashara ambayo mtu atafanya bila kuhitaji fedha. Ndani ya mpango kutabainishwa ni kiasi gani cha pesa unahitaji ili kuweza kutimiza malengo uliyojiwekea. Na pia itaonyesha ni kiasi gani cha pesa utaingiza baada yaw ewe kuwekeza fedha.
 
Bila kujua unachohitaji ni vigumu sana kutafuta maana hujui hata unachohitaji ili uweze kutekeleza mpango au mradi wako kwa ufanisi. Watu wengi huvutwa kuoanza kuogopa pale wanapoona pengine bajeti ni kubwa kuliko kiasi cha pesa ambayo wamewahi kumiliki katika maisha yao yote.
 
KUVUTIA RASLIMALI.

Sifa na faida nyingine kubwa na muhimu ya kuwa na mpango ni kwamba mpango wenyewe unatabia ya kuvutia raslimali kwa maana ya watu na fedha. Utaona watu wanaanza kukuamini na kuvutika kuweka mikono yao kukusaidia kutimiza kusudi lako kwa njia moja au nyingine.
 
Huwezi kumwambia mtu kuwa unafanya biashara au unataka kufanya biashara fulani bila kuwa na mpango. Mpango utakutofautisha kati ya watu wanaomaanisha na wale wasiomaanisha kabisa. Kuna watu wengi sana duniani hawamaanishi na hivyo hawaaminiki.
 
Kuishi,kufanya biashara,mradi au shughuli yoyote bila kuwa na mpango ni sawa sawa kabisa na kuishi bila kujua unaoelekea na hakuna hatari kubwa duniani kama mtu kuishi bila kuwa na mwelekeo.
 
Huwezi hata siku moja kutumbukia kwenye maisha ya mtu ambaye ana mpango na anauishi, kwa nini? Kwa sababu kuna anakoelekea hatakubali mtu mwingine kumwingilia na kuanza kumtumia kwa ajili ya kutekeleza makusudi yao.
 
Mpango unapunguza sana uwezekano wa mtu kupata msongo wa mawazo kwa sababu tafsiri sahihi ya kuwa na msongo ni mtu kutokujua cha kufanya au anchopaswa kufanya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…