Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Ingawa inajulikana zaidi kwa matumizi yake kama burudani ambayo inavutwa au kumezwa, pia imehalalishwa kwa matumizi ya dawa za matibabu katika nchi mbalimbali duniani.
 
Tatifi tatu zilizochapishwa na majarida ya Psychopharmacology, jarida la Neuropsychopharmacology, na International Journal of Neuropsychopharmacology inaonesha jinsi matumizi yake yanavyoweza kuathiri hatua za utambuzi na kisaikolojia.
 
Shirika la Umoja wa Mataifa la Dawa na Uhalifu liliripoti kuwa takriban watu milioni 192 duniani kote kati ya umri wa miaka 15 na 64 wanatumia bangi kwa burudani, kulingana na takwimu za 2018.
 
Hii inaonyesha kuwa watumiaji wengi ni vijana, ambao akili zao bado zinaendelea kukua, jambo ambalo linaweza kuwafanya kupata athari zaidi katika ubongo zinazohusishwa na matumizi ya muda mrefu ya bangi.
 
Tetrahydrocannabinol ndio kiungo kikuu kinachoathiri ubongo katika bangi na eneo linalokwenda kuathiri ni katika mfumo wa endocannabinoid, ambapo kuna vipokezi vinavyoguswa na kemikali vya jani hili.
 
Back
Top Bottom