Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

kucha husaidia kuonyesha afya ya binadamu ipoje yaan kuna baadhi ya Magonjwa dalili zake hujitokeza sehemu mbalimbali katika mwili wa binadamu ikiwemo kwenye kucha... Mfano wa Ugonjwa huo ni UKOSEFU WA KINGA MWILINI, pia ugonjwa wa ini, mapafu na hata moyo
Sawasawa...
 
Jua ni kitu mojawapo ambacho huwa tunakiona kila siku, lakini ni mara chache tumelichunguza.
 
Tafiti mbalimbali zilizofanywa na wataalamu wa afya, zimebaini kuwa kuna manufaa makubwa ya kuota jua angalau kwa kiasi fulani kila siku.
 
Kuua bakteria
Jua linaweza kutumiwa kuua bakteria mbalimbali katika majeraha na ngozi. Tiba hii iligunduliwa na mshindi wa tuzo ya Nobel Niels Finsen. Tiba hii ilitumiwa kuponya vidonda vya wanajeshi wa Kijerumani baada ya vita kuu ya kwanza ya dunia.
 
Huondoa msongo wa mawazo
Inakadiriwa mtu anapokuwa kwenye jua hupata takriban kiasi cha kemikali ya lux kipatacho 100,000. Hivyo kukosa jua kunasababisha tatizo linalofahamika kama vile Seasonal Affective Disorder (SAD) ambayo ni aina fulani ya msongo.
 
SAD hutokea mara nyingi kwa watu wengi kipindi cha masika au kwa wale wanaokaa ofisini muda mrefu. Hivyo kuoata jua kutakuongezea kemikali ya lux na kukuepusha na tatizo la Seasonal Affective Disorder (SAD).
 
Huzuia shinikizo la damu
Utafiti uliofanyika katika chuo cha Edinburgh ulibaini kuwa kemikali ya nitric oxide ambayo hukabili shinikizo la damu, huingia kwenye damu pale mwili unapopigwa jua.
 
Watafiti waliendelea kueleza kuwa kutokana na utafiti huo ni wazi kuwa jua haliboreshi afya pekee, bali hurefusha maisha kwa kumwepushia mtu hatari ya kifo kinachoweza kutokana na shinikizo la damu.
 
Huboresha kinga ya mwili
Tafiti mbalimbali zinaeleza kuwa kukaa kwenye jua la wastani huwezesha uzalishaji wa seli nyeupe za damu ambazo huukinga mwili dhidi ya maradhi.
 
Back
Top Bottom