Lakini kuidhinishwa kwa bidhaa hii ya Eat Just na Singapore kuna uwezekano wa kuwavutia washindani wengine kuanzisha biashara ya aina hiyo katika miji mingine, na inaweza kuchochea nchi nyingine kuidhinisha nyama hiyo ya kuku ya maabara pia .
Shirika la vyakula la Singapore (SFA) limesema kuwa kikundi cha wataalamu kilifanya tathmini ya data kuhusu ulaji wa chakula kilichotengenezwa na kampuni ya Eat Just na kupima usalama wa kuku wa maabara.
" Ilibainika kuwa kuku hao ni salama kwa ulaji kwa viwango vilivyokusudiwa kutumiwa, na waliruhusiwa kuuzwa nchini Singapore kama moja wapo ya bidhaa zilitokana na wazo la thamani au za Eat Just ," SFA ilisema.
Shirika hilo lilisema kuwa limeweka muundo wa udhibiti wa viwango kwa ajili ya "vyakula vipya "ili kuhakikisha kwamba nyama inayotengenezwa kwenye maabara na protini nyinginezo mbadala vinatimiza viwango hitajika kabla ya kuuzwa nchini Singapore.
"Nina uhakika kwamba uidhinishwaji wetu wa nyama inayotengenezwa katika maabara utakuwa ni wa kwanza kati ya wengi nchini Singapore na nchi nyingine kote duniani ," alisema Josh Tetrick, muasisi mwenza wa Eat Just katika taarifa yake kwa vyombo vya habari.
Hakuna dawa za antibiotic zilizotumiwa katika mchakato mzima, na kuku walikuwa na kiwango cha chini cha maikrobaiolojia kuliko kuku wa kawaida, ilisema kampuni hiyo.
"Ni nyama ya kwanza duniani kuruhusiwa na wadhibiti wa viwango , nyama yenye kiwango cha hali ya juu iliyobuniwa kutoka kwa seli ya mnyama kwa ajili ya kuliwa na binadamu ambayo inatoa fursa ya kuanzishwa kwa biashara za kiwango kidogo nchini Singapore siku zijazo," ilisema kampuni ya Eat Just .
Leo May 5, mbunge Kilindi, Omary Kigua ametoa hoja ya kuahirisha shughuli zake za kawaida ili kujadili dharula ya ongezeko la bei ya mafuta. Kigua amesema kuna changamoto ya kupanda kwa haraka sana kwa mafuta ya taa, dizeli na petroli ambapo hivyo vikipanda ni kimepandishwa kila kitu na...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.