Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Unapobaini mteja amepata tatizo kama vile kupata huduma au bidhaa yenye dosari, hakikisha unatafuta njia ya kumsaidia na si kujitetea kuwa mali ikishauzwa hairudishwi au kubadilishwa.
 
Hakikisha unatoa huduma na bidhaa unazotozitangaza na kuzielezea kuwa zipo kwenye biashara yako. Kwa mfano siyo sawa kusema unauza mchele safi lakini ukauza mchele uliojaa chuya au mawe. Au kujinasibisha Kuwa unatoa huduma 10 kumbe zinazopatikana ni mbili tu.
 
Ikiwa biashara yako inahudumia wateja kwa wingi andaa utaratibu wa kuajiri watoa huduma zaidi ili kupunguza foleni kwa wateja.
 
Pokea maoni na mrejesho
Biashara nyingi hazifahamu umuhimu wa kupokea maoni au mrejesho kutoka kwa wateja, na hii ndiyo sababu si jambo la kawaida kuona biashara nyingi za kiafrika zikipokea mrejesho kutoka kwa wateja.
 
Unapojijengea utaratibu wa kupokea maoni na mrejesho kutoka kwa wateja utabaini changamoto zinazowakabili wateja ili uziboreshe pamoja na kufahamu wateja wanapendekeza au wanahitaji ufanye maboresho gani. Kupitia maoni na mrejesho kutoka kwa wateja utaweza kubaini ikiwa mipango na mbinu zako za mauzo na utoaji huduma kama zina ufanisi au la.
 
Matumizi stahiki ya teknolojia yatakuwezesha kutoa huduma nzuri kwa wateja ambayo wataifurahia na kuona thamani halisi ya pesa yao.
 
Ukiwa kama mfanyabiashara anayejali suala la kutoa huduma bora kwa wateja ni lazima uweke utaratibu wa fidia na kuomba radhi pale ambapo jambo fulani halikwenda sawa kwa mteja.
 
Back
Top Bottom