Numbisa
JF-Expert Member
- Dec 12, 2016
- 348,970
- 1,252,247
Kweli...Ukitazama kwa makini pia utabaini kuwa hii ni moja ya sababu inayofanya baadhi ya wafanya biashara kuuza bidhaa bandia au kwa njia ya ujanja ujanja ili tu wapate pesa.
Sawasawa.....Unapobaini mteja amepata tatizo kama vile kupata huduma au bidhaa yenye dosari, hakikisha unatafuta njia ya kumsaidia na si kujitetea kuwa mali ikishauzwa hairudishwi au kubadilishwa.
Hili ni sahihi kabisa..Hakikisha unatoa huduma na bidhaa unazotozitangaza na kuzielezea kuwa zipo kwenye biashara yako. Kwa mfano siyo sawa kusema unauza mchele safi lakini ukauza mchele uliojaa chuya au mawe. Au kujinasibisha Kuwa unatoa huduma 10 kumbe zinazopatikana ni mbili tu.