Zingatia burudani
Burudani tena? Ndiyo, unaweza kubeba miziki ambayo itakuburudisha wewe pamoja na wale unaosafiri nao ili msichoke muwapo safarini. Kusikiliza mziki wakati wa kuendesha gari kutakuweka katika hali (mood) nzuri sana.
Fahamu vyema eneo unalokwenda
Je unafahamu vyema barabara utakayoitumia kufika kwenye eneo unalokwenda? Ili kuepuka kupotea au kukwama kwenye safari yako, ni muhimu ukafahamu vyema eneo unalokwenda.