Yapo mawe yenye muundo wa Makanisa, nyumba na hotel na ni eneo linalopendezeshwa kwa kuzungukwa na Maputo juu, Maputo ya rangi tofauti tofauti na kuzidi kuleta mvuto wa macho.
Ni eneo la kuhistoria linalopatikana Central Anatolia, katika mjimbo ya Nevşehir, Kayseri, Aksaray, Kırşehir, Malatya, Sivas na Niğde nchini Uturuki na Miezi ya Julai na Agosti, hufurika watalii kutoka kila pembe ya dunia
Mbali na mawe, kuna maeneo ya kihistoria mengi na pembeni kumezungukwa na huduma zote muhimu kuanzia uwanja wa ndege, mahotel makubwa na huduma za afya.
Ili kukifikia kisiwa hicho unatumia boti, ndege za majini ama helkopta kutoka fukwe jirani ya Airlie Beach, bandari ya Shute au kisiwa jirani cha Hamilton.
Inatajwa kwamba, ndiyo fukwe iliyopigwa picha zaidi duniani, karibu mitandao na tovuti nyingi za picha kwa upande wa picha za fukwe basi zimekusanya picha kutoka fukwe hii.
Upekee wa fukwe hii ni kwamba hata jua liwake namna gani, mchanga wake hauwi wa moto, haushiki joto, hauunguzi na kufanya uweze kutembea peku ama kulala kwenye mchanga bila shaka yoyote na kufurahia mandhari ya maji na mawingu ya blue kando ya maji.
Pamoja na uzuri huo na pia mchanga wake kutumika kwa ajili ya kusafisha vito vya thamani kama vya madini, mchanga wake unaweza kuharibu vitu vya umeme kama simu na kamera.
Unaweza kuwa umewahi kuona mabwawa mengi ya kuogelea, yapo ya asili na yapo ya kutengenezwa ambayo utayaona mengi kwenye majumba ya watu ama mahoteli makubwa.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.