Mambo muhimu ya kukusaidia kuwa na furaha muda wote
1. Kuwa na uwezo binafsi wa kuvikagua vile ulivyonavyo ndani ya moyo wakoKatika maisha yetu ya kilasiku hatuna budi kujifunza namna ya kujikagua sisi wenyewe, kuvikagua vile tulivyonavyo ndani yetu kwa sababu ni ukweli kwamba pasipo kujikagua sisi wenyewe basi hatutaweza kutambua upungufu tulionao na kama hatutotambua upungufu huo basi hautoweza kushughulikiwa na kuondolewa, maana yake ni kwamba tutazidi kuishi na upungufu wetu na hivyo kuathiri ufanisi wetu na mwisho wake mafanikio yetu kwa ujumla yataathirika.
Nikupe mfano wa mtu mwenye duka, mara kwa mara mmiliki wa duka huwa na muda wa kuvikagua vitu au mali aliyonayo dukani (stock taking) na hapa huweza kutambua nini kimepungua, nini hakipo kabisa na nini kipo kwa wingi.
Jifunze kufanya tathmini ya maisha yako binafsi kila wakati, tathmini matendo yako ya kila siku, maneno yako ya kila siku, mitazamo yako halafu angalia wapi kuna upungufu na wapi kuna fursa zaidi.
Baadhi ya maeneo ya upungufu ambayo tunaweza kuwa nayo katika maisha ni kama vile upungufu wa kihisia, kiroho kiujuzi , kifedha na mengineyo mengi. Kumbuka, uzuri ni kwamba kila tunapoweza kutambua upungufu tunaziona fursa za kuweza kuushughulikia.
Wengi wetu tumeshindwa kuyafikia malengo tuliyowahi kujiwekea kwa sababu tu hatunamisimamo katika vile tunavyoviamini , kwa hiyo inakuwa rahisi kuyumbishwa na kupeperushwa na kila upepo unaokuja upande wetu.
Ili kufikia mafanikio tunayoyatamani hatuna budi kuwa na misimamo fulani katika maisha. Naupenda msemo unaosema kama huwezi kuwa na msimamo katika chochote basi utachukuliwa na chochote.
Ni vyema kufahamu kila wakati maishani kuwa kama hauna msimamo katika ufanisi basi utaangukia katika uzembe na kutowajibika na kama hautakuwa na msimamo katika kuhakikisha unafanikiwa basi utaangukia katika umaskini.
Amua mwenyewe ninini unasimamia na ni wapi unaiweka misimamo yako kwa sababu vile tunavyoamua kuwa na misimamo navyo ndivyo vinavyosimama kama misingi katika maisha yetu.