Haya ni baadhi tu ya mambo ambayo unaweza kujifunza au kuyapata kutoka kwenye vitabu. Hivyo ikiwa unataka kuwa bora zaidi jizoeze kusoma vitabu mbalimbali kila mara.
Ikiwa unataka kuongeza wigo wako wa maarifa na fursa, basi huna budi kujifunza lugha mpya. Ikiwa unafahamu Kiswahili pekee, basi jifunze Kiingereza pia.
Jifunze kozi mpya
Je kuna kozi mpya unayoweza kujifunza? Ikiwa ipo, chukua muda sasa ujifunze kozi hiyo. Kujifunza kozi mpya kutakuongezea maarifa na uelewa wako.
Boresha ujuzi wako
Je kuna maarifa au ujuzi fulani ulio nao? Je kiwango na ubora wake kikoje? Ikiwa una ujuzi fulani hakikisha unaukuza na kuuendeleza uwe bora kabisa.
Ikiwa wewe ni mjasiriamali, mbunifu, fundi, msanii n.k. Hakikisha unajenga uwezo na maaraifa yako yawe bora kabisa. Kila mara hakikisha unajifunza mambo mapya yanayohusiana na ujuzi wako.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.