Epuka watu walioshindwa
Mara nyingi tunazungukwa na watu walioshindwa kuliko wale waliofanikiwa. Watu hawa wamejaa maneno mengi yenye visingizio na kulaumu kila kitu.
Hivyo hatuna budi kuwaepuka watu hawa ili wasije wakatukwamisha katika kufikia malengo yetu. Ili kuwa bora zaidi ni muhimu kutambua ni watu gani wakuwa karibu nao maishani mwetu
Ni muhimu kutenga muda wa kutosha wa kupumzika ili tuweze kuwa bora zaidi. Kumbuka gari haliwezi kwenda bila kuwa na mafuta; nguvu na afya njema ndiyo mafuta ya miili yetu.