Utafiti uliofanyika katika chuo cha Edinburgh ulibaini kuwa kemikali ya nitric oxide ambayo hukabili shinikizo la damu, huingia kwenye damu pale mwili unapopigwa jua.
Watafiti waliendelea kueleza kuwa kutokana na utafiti huo ni wazi kuwa jua haliboreshi afya pekee, bali hurefusha maisha kwa kumwepushia mtu na hatari ya kifo kinachoweza kutokana na shinikizo la damu.
Inafahamika wazi kuwa jua ni chanzo cha upatikanaji wa vitamini D ambayo huuwezesha mwili kufyonza madini ya calcium na phosphorus yanayoimarisha mifupa.
Inaelezwa pia vitamini D3 inayozalishwa wakati wa uzalishaji wa vitamini D, husaidia kuzuia kuvunjika kirahisi kwa mifupa hasa kwa watu wenye umri mkubwa.
Katika utafiti mmoja uliofanyika kwa watu wenye matatizo ya ngozi, ulibaini kuwa asilimia 84 ya magonjwa hayo yalipona baada ya kukaa kwenye jua kwa muda uliopendekezwa na daktari.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.