Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Ukweli ni kwamba sio kuwa wao wanasiri nyingi za kufanikiwa kuliko wewe bali ni misimamo thabiti waliojiwekea ili kuendana na ukuaji wa changamoto za maisha
 
James William (Harvard University ) aliwahi kusema kwamba " A human being can alter their lives by altering their attitude of mind" akiwa anamanisha kwamba binadamu yeyote anaweza kupunguza maisha yake kwa kupunguza musimamo wa fikira zake.
 
Mafanikio yoyote hayapimwi kwa kipato ulichonacho bali pia katika hisia, misimamo na mahusiano juu ya watu wanao kuzunguka
 
MSIMAMO WAKO HUCHANGIA MAFANIKIO YAKO:

Neno msimamo ni muhimu sana katika nyanja yoyote ya mafanikio. Kwa mfano
Mtendaji yeyote kwenye kampuni anaweza kuwa mzuri bila kuwa na msimamo?
Mwanafunzi yeyote anaweza kuwa mzuri darasani bila kuwa na msimamo? , Mzazi., Mwalimu, mfanya biashara, mwajiri, mwajiriwa nk wanaweza kuwa na utaratibu mzuri wa sheria bila kuwa na msimamo? .
Kwahiyo kuwa na msimamo kwenye maisha yako kuna harakisha mafanikio yako mbele zaidi.
 
KUWA NA MSIMAMO KUTAKUSAIDIA KUTATUA MATATIZO (NYUMBANI NA KAZINI KWAKO)

Ukiwa na msimamo ni rahisi sana kuwepukana na musongo wa mawazo katika maeneo mbalimbali kama vile kwenye familia pamoja na maeneo unayofanyia kazi zako. Lazima tukubaliane kwamba sisi sote ni watu wa majukumu tunakwenda kujitafutia riziki na tunarudi nyumbani.
 
Kinachotokea ni kwamba asilimia kubwa ya watu huchukua matatizo ya kazini na kurudi nayo nyumbabi na pia huchukua matatizo ya nyumbani na kwenda nayo kazini
 
Kinachotokea unapokuwa unahama na matatizo ni kwamba uzalishaji utapungua na musongo wa mawazo utaongezeka kazini kwako. Hivyo hivyo kwenye familia. Hiyo yote ukiwa na msimamo ni rahisi kujua namna ya kuvitatua
 
ujuzi : Tabia zetu zina badilika kutokana na ujuzi wa watu mbalimbali tunaokutana nao katika maisha yetu. Watu tunaokutana nao kila siku katika maisha huweza kubadili kabisa misimamo yetu kutoka chanya na kuwa hasi au kutoka hasi na kuelekea chanya. Hii inategemea sana na aina ya watu tunao changamana nao.
 
Back
Top Bottom