Numbisa
JF-Expert Member
- Dec 12, 2016
- 348,970
- 1,252,247
Huongeza ubora
Toa mwongozo mkuu tufanyeje isitokee.. mimi inanikuta Sana hii kukunjana na makonda wa daladala asb ni jambo la kawaida.Kinachotokea ni kwamba asilimia kubwa ya watu huchukua matatizo ya kazini na kurudi nayo nyumbabi na pia huchukua matatizo ya nyumbani na kwenda nayo kazini
Anasa ni kitu kibaya Sana katika maishaBaada ya kuwa tumeangalia kwa uchache juu ya kuwa na msimamo thabiti, sasa tuangalie kidogo badhi ya mambo ambayo hufanya watu wengi kutofanikiwa kwa haraka kwenye maisha yao.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Rafiki yetu mmoja ametuambia kwenye group jingine kuwa kuna sokomoko limetokea nyumbani kwake na moto wake hauzimiki leo ni wiki ya tatu na mwisho wake haujajulikana bado... Sokomoko hilo lilianza hivi... Jamaa aliweka Picha ya gari lake la zamani na kuweka maneno ya status "Baya kama nini, hata kuliangalia linatia kinyaa" kwa bahati mbaya au nzuri mke wake wakati huo wote simu yake Ilikuwa inasumbua hivyo hakuweza kuingia watsap. Baada ya kama wiki akaweka Picha ya mkewe alafu akasahau kuondoa maneno ya status iliyokuwa na Picha ya ile gari... Shetani anavyojua kuyapanga mambo, simu ya mkewe ikatengemaa akarudi hewani na kukuta Picha yake kwenye profile ya mumewe na maneno yale... Mpaka leo nyumba haijatulia