Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Paris St-Germain ilimpa mshambuliaji wa Brazil Neymar, 30, kwa Manchester City ili kubadilishana na kiungo wao wa kati wa Ureno Bernardo Silva, 27, lakini mabingwa hao wa Premier League walikataa mpango huo. (Le Parisien - in French)
 
Chelsea wanakaribia kuafikiana na Sevilla kwa kitita cha pauni milioni 60 kumnunua mlinzi wa Ufaransa Jules Kounde, lakini huenda wakakabiliana na ushindani kutoka kwa Barcelona kuwania saini ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23. (Guardian)
 
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33 alikuwa amesalia na mwaka mmoja katika mkataba wake na mabingwa hao wa Ujerumani lakini mwezi Mei alisema: "Hadithi yangu na Bayern imekwisha.".
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…