Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Arsenal wanapanga kumtambulisha Oleksandr Zinchenko kama usajili mpya. Inaelezwa ameondoka kwenye kambi ya Manchester City, ili kufanya vipimo na kujiunga na kambi ya Arsenal (Fabrizio Romano).
 
Lingard yuko huru baada ya mkataba wake na Manchester United kumalizika June 30, 2022. West Ham pia inaendelea na mazungumzo ya kumnasa mshambuliaji wa Chelsea Armando Broja. Skysport
 
Juventus imefikia makubaliano na Torino kuhusu uhamisho wa Gleison Bremer! ada ya €40m imekubaliwa na Torino kwa ajili ya beki huyo wa kati huyo Mbrazil aliyekuwa anasakwa pia na Inter (Fabrizio Romano).
 
Afisa mkuu Mtendaji wa Bayern Munich Oliver Kahn amemtaja mshambuliaji wa Tottenham na Uingereza Harry Kane, 28, kama "mshambulizi bora kabisa" na "ndoto ya siku zijazo" baada ya kukubali kumuuza Robert Lewandowski, 33, kwa Barcelona. (Star)
 
Barcelona wameelekeza nguvu zao kumleta mlinzi wa Sevilla na Ufaransa Jules Kounde, 23, ambaye pia amekuwa akihusishwa na Chelsea, baada ya kufikia makubaliano ya kumnunua mshambuliaji wa Poland Lewandowski. (Marca)
 
Tottenham wako tayari kulipa euro 17m (£14.4m) kwa mshambuliaji wa Barcelona Memphis Depay, lakini klabu hiyo ya Uhispania inataka euro 20m (£17m), ingawa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 pia anasita kuondoka Nou Camp. Sport - in Spanish)
 
Back
Top Bottom